Sisi katika Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu tunaiangalia India kama nchi ya kisasa inayoendelea ili kusonga mbele zaidi

Sisi katika Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu tunaiangalia India kama nchi ya kisasa inayoendelea ili kusonga mbele zaidi

Marafiki Zangu: 

 Nilisubiri kwa hamu fursa hii ya kuona Bwawa la Bhakra, ambalo ndugu wa Bwawa la Juu huko Jamhuri ya Muungano ya Kiarabu, pia ninathamini sana juhudi nilizoziona leo na mikono inayojenga bwawa hilo.

Ninahisi kuwa kipindi cha Ukoloni mliyopitia hapa India mlikuwa mnahitaji malighafi zenu zote ; kufukuza Ukoloni huo na kupata uhuru, lakini sasa jukumu likawa kubwa zaido kuliko hilo,  Tunataka shauku, tunahitaji kazi na ustahimilivu, leo nilipitisha kiasi cha mawazo ambayo mliyapitisha, na kiasi cha kazi ya bidii mlidhamiria kufanya na kusimamia.

Pia nathamini juhudi na mtindo mliyofuata kujenga nchi yenu mara tena ,na nchi kadhaa zinawaangalia kama ni mfano bora wa kufuata mtindo huo.

Basi sisi katika Jamhuri ya Muungano ya Kiarabu  tunaangalia India kama nchi ya kisasa inayojiboresha kwa ustawi , pia ni nchi inayojaribu kwa njia tofauti kupata maendeleo ili kulinda kazi zake na vifaa vyake ili kufidia kile kilchoipit zamani.

Nchi za Afrika na Asia zote zinaangalia India  kama mfano wa kujitegemea kwa Siasa, na inajaribu kutekeleza na kuthibitisha sera ya kujitegemea na pia inajaribu wakati huo huo kujiboresha ili kufikia Maendeleo na Ustawi .

Kwa hivyo, tunajaribu pia kufaidika kutoka uzoefu huo; kwa sababu tunaweza kufaidika kutoka kwa uzoefu wote ambao India imepitia,na nchi zilizopata uhuru hivi karibuni katika Afrika na Asia zinzowaangalia kama mfano mzuri na wa kuigwa.


Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika kutembelea Bwawa la Bhakra kaskazini mwa Punjab.

Mnamo Aprili mosi, 1960.