Misri haina nia yoyote ya Uadui 

Misri haina nia yoyote ya Uadui 

Swali la Mhoji:  Mheshimiwa Je, unaweza kufafanua mazingira ya mkataba wa mwisho wa silaha? 

*Rais Nasser: Nilisoma katika magazeti ya Marekani uchambuzi makini wa msimamo wetu, ambapo ulielezwa kama kuwa Israel itaweza daima kushinda nchi za Kiarabu isipokuwa Misri inaweza kununua silaha kutoka Urusi,na nilifuata ushauri huu wa busara  wa Marekani ,kwa hivyo nikamuuliza balozi wa Urusi hapa ikiwa Umoja wa Kisovieti uko Tayari kutuuzia silaha, na nilidhani jibu litakuwa hamna, lakini balozi alinijibia baada ya siku nne na kuniambia kuwa wako tayari. Na nilipomjulisha balozi wa Marekani huko Kairo kuhusu hili; Alifikiri kwamba hii ilikuwa ni ovyo, na akasema kwamba hii ni hila iliyokusudiwa kulazimisha Amerika kuuza silaha kwa Misri. 

Hiyo ilikuwa tarehe 9 Juni iliyopita, na tarehe 12 Juni, balozi wa Uingereza aliniambia kwamba ikiwa tutanunua silaha kutoka kambi ya mashariki, Uingereza itakataa kutupatia silaha yoyote. 
Nilimjibu kwamba hii ilikuwa tishio, na niliwasiliana na Warusi, na ikiwa Uingereza itatekeleza tishio lake, hii haitatuacha chaguo ila kugeukia kambi ya mashariki. 

Waingereza hawakutekeleza tishio lao, lakini tangu siku hiyo hadi tarehe 27 Septemba--siku  niliyomwambia Balozi wa Uingereza kwamba tumefanya mkataba  wa silaha pamoja na Chekoslovakia-hakukuwa na majadiliano kati yetu na Magharibi kuhusu silaha. 

Swali la Mhoji : Je, kuna uwezekano wa mataifa makubwa kuingilia kati ya hali iliyopo? 

* Rais Nasser: Imani yetu katika nia yenu nzuri ni ndogo sana kwa wakati huu, na ninaogopa kwamba watetezi wa Israeli katika bunge lenu watakuwa wengi sana, basi hatutakuwa na uhakika kutoka kwenu.

Swali la Mhoji: Je, kuna uwezekano kwa Misri kuchukua msimamo wa kutoegemea upande wowote? 

Rais Nasser: Tunawezaje kutoegemea upande wowote wakati tumefungwa kwa miaka mingine saba kwa makubaliano na Uingereza katika Mfereji wa Suez?! Si suala la kutoegemea upande wowote, bali la kutotawaliwa na nchi ya kigeni. 

Swali la Mhoji: Ni Nini nia yenu kwa Israeli? 

*Rais Nasser: Misri haina nia yoyote ya Uadui, na mashambulizi yote yaliyotokea tangu kumalizika kwa vita vya Palestina hadi sasa yalitoka kutoka upande wa Israel, na hatukuanza kujibu mapigo isipokuwa tangu Agosti iliyopita tulipotoa amri la kufanya hivyo. 

Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kwa jarida la "Daily Herald", gazeti la Chama cha Wafanyikazi cha Uingereza.

 Novemba 8,1955.