Kwanini Mheshimiwa Rais mnawashambulia waingereza Barani Afrika?

Kwanini Mheshimiwa Rais mnawashambulia waingereza Barani Afrika?

Swali la Mhoji: kwanini Mheshimiwa Rais mnawashambulia waingereza Barani Afrika? Tunasikia kutoka kwa redio ya Kairo hasahasa kupitia sauti ya Afrika huru -kuhusu utawala wetu wa kikoloni, tena nadhani kwamba wapo wanaokubaliana nasi kwamba kwa ujumla tunafanya kazi yetu vizuri kabisa, kama uhuru wa Ghana na Nigeria na mazungumzo yanayojiri kuhusu Kenya, Nyasaland na nyingine.

Rais Nasser : Hatuwashambulii , bali tunashambulia ukoloni, Tunasimamia dhidi ya ukoloni na tunahimiza haki ya kujitawala na uhuru kwa nchi zote.

 Na kama mnasema nchi yenu ni moja ya nchi huru Duniani; basi mwishoni vitendo ndivyo vyashinda maneno , na sio kauli mbiu bali ni sera zinazotekelezwa.

-Swali la Mhoji  : lakini je , hufikiri kwamba tunachangia sana kuelekea uhuru na kujitegemea kwa nchi hizo Barani Afrika ?

Rais: Nyinyi -kwa mfano- mnapomfukuza kiongozi wa Kenya na mnaweka viongozi wa nchi nyingine gerezani, basi hamfanyi vizuri kabis. Nilikutana na kiongozi mmoja Nyasaland ambaye alikuwa anarudi kutoka London, na alipofika alikamatwa.
                                   
Sehemu ya mahojiano ya Rais kwenye televisheni na "Woodrow White".

Mwakilishi wa televisheni ya Uingereza mnamo Septemba 3, 1960.