Ujumbe wa Tunisia unaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa hukutana na Balozi wa Jamhuri ya Tunisia kwa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri

Imetafsiriwa na: Menna Ashraf Ragab
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Mheshimiwa Balozi wa Jamhuri ya Tunisia kwa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mheshimiwa Mohamed Ben Youssef, na Ambatisha ya Utamaduni, Bi. Amira, walipokea ujumbe wa Tunisia unaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ulioandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo chini ya kauli mbiu "Ushirikiano wa Kusini-Kusini" chini ya Ufadhili wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, wakati wa kipindi cha 1 hadi 16 Juni 2021, na pamoja na ushiriki wa viongozi vijana 120 katika mabara matatu (Afrika - Asia - Amerika ya Kilatini), mkutano huo ulijadili umuhimu wa vijana katika kujenga jamii, hasa jukumu lililochezwa na vijana katika diplomasia ya umma.
Mheshimiwa Balozi Mohamed Ben Youssef aliongeza kuwa amekuwa akifuatilia shughuli zote za ujumbe wa Tunisia tangu siku ya kwanza ya ufunguzi na alionesha nia yake ya dhati katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, unaostahili makada vijana wenye uwezo wa kuchukua nafasi za uongozi katika nchi mbalimbali, ambayo huongeza ushirikiano wa kimataifa wa Tunisia na Misri.
Kwa kumalizia, Mheshimiwa Balozi alielezea msaada wake endelevu kwa vijana wa Tunisia, ambao daima huangaza na kuinua bendera ya kitaifa pamoja na nchi 53 kutoka duniani kote.
Tunawatakia mafanikio na ufanisi washiriki wote kwa faida ya nchi yao na ardhi zao.