Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Chad ni Mkuu wa Rasilimali ya Watu katika Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Afrika

Kiongozi wa Chad " Mohamed Haroun," Mratibu wa Harakati ya Nasser kwa Vijana huko Jamhuri ya Chad, na mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alichaguliwa kuwa mkuu wa Mamlaka ya Rasilimali ya Watu, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Baraza la kiuchumi na Kijamii linalohusiana na Umoja wa Afrika, hayo yalitokea wakati wa uchaguzi uliofanyika jana jioni huko mji mkuu wa Kenya, Nairobi, baada ya kupata uungaji mkono wa wawakilishi wa nchi za Afrika kwa pamoja katika Baraza ili kuiwakilisha Chad kwa miaka minne ijayo katika mamlaka hiyo.
Katika muktadha huo huo, inaashiriwa kuwa Mamlaka ya Rasilimali ya Watu na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ina Sehemu nne (Elimu, Teknolojia ya Habari, Vijana, Rasilimali ya Watu na sayansi ya teknolojia ya kisasa) na Baraza la kiuchumi , kijamii na kiutamaduni linazingatiwa kama mamlaka ya Ushauri kwa Umoja wa Afrika inayolenga kutumia vyema ujuzi wa mashirika ya kijamii na kupaza sauti yake kupitia kutoa ushauri ndani ya taasisi za Umoja wa Afrika na michakato ya kutunga maamuzi, kwa nia ya kutekeleza malengo, kanuni na sera za Umoja huo katika programu yenye ufanisi na katika hali halisi.
Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ulizinduliwa mnamo Julai 2019 kama Udhamini wa Kiafrika - Kiafrika, wakati wa uongozi wa Misri kwa Umoja wa Afrika. Chad ni mojawapo ya nchi za awali zilizoshiriki, na baada ya kuhitimu wakaanzisha tawi la taifa la Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Chad, na waliweza wakati wa miaka minne ,kuzindua programu kadhaa za Vijana, mipango ya Jumuiya na kozi za mafunzo, ikiwa ni pamoja na kufunza vijana wa kiume na wa kike 1,800, katika mikoa 6, ikijumuisha: “Wadi Absha” na Shari El-awst “Saar”, Hajar Lamis “Al-Maqat” na Batha “Umm Hajar” pamoja na mji mkuu, Njamena. vilevile , kundi la Harakati ya Nasser kwa Vijana huko Chad limesifiwa moja kwa moja kutoka kwa Rais wa Jamhuri" Mohamed Idriss Deby" , wakati wa ushiriki wao katika Kongamano la Kitaifa la Vijana la Chad mnamo Desemba 2021 ambapo walitoa takriban mapendekezo 44, la kwanza likiwa ni kupitishwa kwa Mkakati wa Kitaifa wa Vijana, na kuwaunganisha katika vituo vya kutunga maamuzi.