Kwa mahudhurio ya Rais wa Uganda .. Ghazaly ni mzungumzaji katika Mkutano wa Bara kwa vijana wenzake
Kiongozi kijana "Hassan Ghazaly", Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, alishiriki kama mzungumzaji katika Mkutano wa Vijana wa Mechanism ya Afrika kwa pitio la marafiki katika toleo lake la tatu, uliofanyika kuanzia Julai 4 hadi 9, 2022, katika Hoteli ya Speke Munyonyo huko mji mkuu wa Uganda, Kampala, ukiwa na kauli mbiu "Kurekebisha Mwenendo wa Mpango wa Vijana kwa Bara lenye Mabadiliko", na hivyo kwa mahudhurio ya kundi la viongozi watendaji na watoa maamuzi wa Umoja wa Afrika na serikali ya Uganda, wakiongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Rais Kaguta Museveni, Waziri Mkuu wa Uganda, Bi. Rubina Nabanya, na Makamu wa Rais wa Baraza la Taifa la Vijana la Uganda, Bi. Esther Nankia, na Mshauri wa Rais wa Uganda kuhusu Masuala ya Vijana Bw.Daniel Opal , Mjumbe wa Vijana wa Umoja wa Afrika, Bi. Chido Mbemba, na Afisa wa Faili za Vijana, Sekretarieti ya Bara ya Mfumo wa Afrika kwa pitio la marafiki, Bw. Lennon Meunier, Pamoja na ushiriki wa viongozi vijana 800 kutoka barani kote Afrika, Asia na Ulaya.
Katika muktadha huu, ushiriki wa Ghazaly ulikuwa kama mwakilishi wa Misri na mzungumzaji katika kikao chenye kichwa "Jukumu la Vijana katika kufikia Mpito wa Nishati wa Haki na Usawa," ambapo alijadili njia ya COP27, na dhana ya haki ya hali ya hewa, na umuhimu wa kuwawezesha vijana kuchukua hatua za tabia nchi, na kufaidika kutoka mawazo yao na kuwekeza nguvu zao.
Mwanzoni mwa mazungumzo, Ghazaly aliwasilisha salamu za dhati za Misri kwa watu wa Uganda na hadhira wote, aliendelea kueleza kuwa faili ya hali ya hewa ni kipaumbele cha juu kwa taifa la Misri, na kwa kuzingatia mipango yake, inachukua hatua na taratibu nyingi kushirikisha na kuwawezesha vijana katika hatua za hali ya hewa kwa kutumia mawazo yao ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuimarisha ushiriki wao katika COP27, na akisisitiza kuwa Misri inafanya kazi ya kuchukua sauti za vizazi vijavyo vya vijana na watoto katika mchakato wa kufanya maamuzi kuhusiana na suala hili, kama kichocheo bora cha kufikia matokeo halisi, yanayowezekana na yanayotekelezeka.
Ghazaly pia aliashiria kuwa Misri, wakati wa maandalizi yake ya mkutano wa hali ya hewa wa COP27, ina mihimili miwili mikuu: Elimu na Mwanadamu, Wakati wa maandalizi hayo, ilijali kikubwa ushiriki wa Wizara, mashirika na wanaohusika faili hili ndani ya nchi, pamoja na nia yake kamili ya kuhusisha mashirika yote ya Jumuiya ya kimataifa katika tukio hilo la kimataifa kwa kuzingatia urais wake wa mkutano ujao wa hali ya hewa.
Ghazaly alihitimisha hotuba yake, "Misri ni kijiji changu... Afrika ni mji wangu" katika ujumbe kwa vijana wenzake akisisitiza umuhimu wa kushirikiana pamoja na taifa moja ili kuunganisha sauti ya Afrika na kufafanua mahitaji ya bara, na Kuunda nafasi inayohakikisha uhamasishaji wa sauti za wanawake na vijana, na katika kukabiliana na changamoto za hali ya hewa,katika maandalizi ya matokeo ya Mkutano wa Hali ya Hewa wa Sharm El-Sheikh COP 27, kufuatilia matokeo yake na kuyaunganisha na ukweli,kutokana na nafasi yao muhimu katika mafanikio ya juhudi za kimataifa za kushughulikia suala la mabadiliko ya hali ya hewa, na mchango wao kwa makusudi katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
 
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
                                        
                                     
            
            