Harakati ya Nasser kwa Vijana ni Msemaji rasmi huko Dodoma wakati wa sherehe za kitaifa za kumbukumbu ya Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Harakati ya Nasser kwa Vijana ni Msemaji rasmi huko Dodoma wakati wa sherehe za kitaifa za kumbukumbu ya Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwa mwaliko rasmi wa Wizara ya Elimu ya Juu kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, "Menna Yasser" mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na mratibu rasmi wa idara ya lugha ya kiswahili wa harakati ya  Nasser kwa Vijana ameshiriki katika maadhimisho ya kitaifa ya kumbukumbu ya  miaka 61 ya uhuru wa Tanzania, yaliyofanyika jana jioni huko mji mkuu  wa nchi, Dodoma, kama mmoja wa Vijana wanamitindo wa Misri mashuhuri na maarufu, na hiyo kwa mahudhurio ya maafisa wakuu wa serikali wakiwemo wanadiplomasia, watoa maamuzi na wataalamu wa vyombo vya habari, mbali na viongozi watendaji kutoka sekta mbalimbali nchini, na mbali na mashirika makubwa ya habari ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Idhaa ya Ujerumani "Deutsch Welle" na Shirika la habari la "BBC" kwa Kiswahili.

Mwanzoni mwa hotuba yake, Yasser alielezea furaha yake kwa mwaliko wa kushiriki katika kongamano muhimu la kitaifa, akiashiria kuwa jambo hilo lina maana kubwa kwake, ambapo anaalikwa kila mwaka kusherehekea tukio hilo hilo huko Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, lakini mwaka huu anaalikwa kuhudhuria na kushiriki katika mji mkuu, Dodoma sanjari na muda wa uwepo wake kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia alieleza kuwa dhana ya Umoja wa Afrika inayotetewa na viongozi wa Afrika daima imekuwa kama ndoto ya kuhakikishwa katika hatua na misimamo halisi, na akibainisha kuwa mwaliko wake kwenye Jukwaa la Kitaifa ni mojawapo ya mifano ya kuhamasisha vijana, ilimfanya achukue jukumu lake mwenyewe kufungua upeo mkubwa kwa wenzake vijana,  akisisitiza kuwa lugha hiyo ni ulimi  wa watu, ambao naye hujitahidi kupitia lugha ya Kiswahili kuwafikia watu wengine katika maeneo mapana ya bara hili na hata nje ya bara hilo, kusambaza utambulisho na historia yao na kuwawakilisha mbele ya ulimwengu kwa hali ya juu binafsi na kujiamini katika mustakabali mzuri wa bara lao, wakichukua kauli mbiu "Kama sio sisi, basi nani! .. Ikiwa sio leo, basi lini?" Mfano wa matumaini ya watu wa Afrika tunalolitaka. 

Maisha ya "Menna Yasser" yanajaa ushiriki mwingi wa jamii katika kuunga mkono vijana haswa miongoni mwa wanafunzi, naye ni mmoja wa wanaharakati wa kike wenye ushawishi mkubwa katika uwanja wa masomo ya Kiafrika, basi ana michango mingi ya kiutamaduni na kiakili katika lugha za Kiarabu na Kiswahili, ndio maana yeye ndiye mmisri wa kwanza kuchapisha kitabu katika lugha ya Kiswahili "NJIANI" katika uwanja wa kujiendeleza na maendeleo ya mwanadamu,  mbali na programu zake tajiri za redio kwenye  online redio, pia  ni mtafiti wa uzamili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Tanzania, Hivi karibuni alijiunga na Kitivo cha Mafunzo ya Kiafrika ya juu, Chuo Kikuu cha Kairo, kupata digrii ya uzamili katika Isimu (Kiswahili), mnamo 2019 alijiunga na Mpango wa Kujitolea wa Umoja wa Afrika, Kisha akafanya kazi kama mhadhiri wa Kiswahili katika kampuni ya "Community of Babel" Pia anafanya kazi kama Mkurugenzi na Afisa wa Lugha ya Kiswahili katika moja ya sekta ya matibabu huko Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mbali na kazi yake kama mtafsiri wa lugha ya Kiswahili katika Ofisi ya Vijana ya Afrika - Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri, kuanzia 2018 hadi sasa.

Ikumbukwe kwamba Harakati ya Nasser kwa Vijana inathamini juhudi za vijana wake miaka minne baada ya kuanzishwa na inajivunia hatua za ujasiri zinazochukuliwa na viongozi na wanachama wake katika njia zao za kitaaluma na kazi zao za uwanjani zina athari kubwa, Harakati hizo pia zina nia ya kufikia dhana ya uendelevu wa programu zinazolenga kuwawezesha vijana, Kiini chake ni Udhamini wa  Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, wahitimu wake kutoka 2019 hadi sasa wameofikia takriban 420, na ukiwekeza katika nguvu za vijana, katika maeneo ya maendeleo na kujenga amani, ujuzi wa kuboresha na kuhamisha uzoefu wa kitaifa, Kama jukwaa la kina kwa vijana wenye ushawishi mkubwa zaidi katika mabara matano (Afrika, Asia, Ulaya, Amerika ya Kusini, Australia), Waratibu wake wanafanya kazi kwa bidii ili kuendeleza wenzao na kuongeza ushiriki wao katika ngazi za kitaifa na kimataifa.