Taasisi ya Gamal Abdel Nasser Nchini Somalia

Taasisi ya Gamal Abdel Nasser Nchini Somalia
Taasisi ya Gamal Abdel Nasser Nchini Somalia
Taasisi ya Gamal Abdel Nasser Nchini Somalia

Imetafsiriwa na/ Sara Saed
Imeharirwa na/ Mervat Sakr 

Misri na Somalia zina mahusiano imara wa kindugu yaliyokita mizizi katika historia, na Misri ilikuwa moja ya nchi za kwanza kutambua Uhuru wa Somalia mwaka 1960, na kutoa msaada kwake katika nyanja mbalimbali baada ya Uhuru. Misri ina jukumu muhimu hadi leo katika kueneza Utamaduni na elimu nchini Somalia kwa kutuma walimu wanaohusishwa na Wizara ya Elimu kufundisha katika shule za Somalia, au walimu wanaohusishwa na Al-Azhar Al-Sharif, pamoja na wataalam wa Mfuko wa Misri wa Ushirikiano wa Kiufundi na Afrika ambao hueneza sayansi katika taasisi za elimu ya juu, na Al-Azhar Al-Sharif inatoa idadi ya Udhamini wa kila mwaka kwa wanafunzi wanaotoka Jamhuri ya Somalia kusoma katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar au Taasisi za Al-Azhar.


Katika miaka ya sitini ya karne iliyopita, Rais Gamal Abdel Nasser aliamuru kuanzishwa kwa taasisi katika mji wa Burao, mji mkuu wa mkoa wa Togdir, mji wa pili kwa Ukubwa nchini Somalia, kuwafundisha ndugu wa Somalia lugha ya Kiarabu na kuwaelimisha, na Taasisi hiyo ni taasisi kongwe zaidi inayofundisha Kiarabu katika Nchi ya Somalia, ambayo hutumika kama nguzo ya kitamaduni katikati ya giza linaloshuhudiwa na serikali hiyo kwa sababu ya vita, vikundi vya kigaidi vyenye silaha, Umaskini na njaa.

Mwanafunzi anasoma kuanzia shule ya msingi hadi mwisho wa shule ya sekondari anayestahili kujiunga na chuo kikuu, na baada ya miaka ya vita nchini Somalia, mifumo ya elimu ilibadilika na hivyo masomo yakawa kwa Kiingereza au Kisomali, lakini masomo katika taasisi hii yalibaki kwa Kiarabu, jambo lililomfanya kuwa na sifa kubwa katika kueneza na kuendeleza lugha ya Kiarabu katika mazingira yanayozunguka.

Taasisi hiyo sasa inafanya kazi na walimu wa pili wa Misri wanaohusishwa na Wizara ya Elimu ya Misri, na inafundisha mitaala iliyotengenezwa nchini Misri kwa kushirikiana na Somalia, ikihitimu mamia ya wanafunzi kila mwaka. 


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy