Siku ya Kiswahili Duniani

Imeandikwa na/ Abdel Moneim Khalifa
Kwa kawaida, kila siku ya Julai 7 hutumiwa kama Siku ya Kimataifa ya kuadhimisha na kusherehekea Kiswahili, lugha inayozungumzwa na watu milioni 250 katika nchi 13. Mnamo tarehe Novemba 23, 2021, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) katika Mkutano wake wa 41 wa nchi wanachama uliofanyika Paris, huko Ufaransa, lilipitisha Julai 7 kuwa siku rasmi ya Kiswahili Duniani. Hii ilifanya Kiswahili kuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika kudumishwa na Umoja wa Mataifa, ni mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Afrika (AU).
Ikiwa hii ni mara ya tatu kwa lugha hiyo kuadhimishwa tangu kupitishwa kwake na UNESCO, maadhimisho mbalimbali hufanyika kwa siku hii, kuanzia Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, kwenye New York, huko Marekani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), SADC (yaani Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika), na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na wizara na serikali mbalimbali kuongoza maadhimisho rasmi katika nchi zao, na kauli mbiu ya mwaka huu ni kuonesha nguvu ya lugha ya Kiswahili katika zama za kidijitali.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO) likiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay, iliyeongoza maadhimisho hayo kutoka Marekani, ikisema "Kiswahili ni lugha inayozungumzwa na watu wa zamani na wa sasa na ni mojawapo ya lugha za Kiafrika zinazotumiwa sana, kama njia ya kawaida ya mawasiliano katika maeneo mengi ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, pamoja na Mashariki ya Kati.
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pia iliandamana kuadhimisha siku hiyo katika mji mkuu Kampala, huko Uganda pamoja na Waziri Mkuu wa Uganda Nabanga Robina, aliyeongoza sherehe hizo.
Nchini Kenya, Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Urithi, Benina Malonza, aliongoza maadhimisho hayo nchini ambapo wadau wengi walikusanyika na kufanya maandamano jijini humo kwa maonesho mbalimbali katika Kituo cha Utamaduni cha Kiswahili. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pia ametuma ujumbe wa pongezi kusherehekea siku ya Kiswahili.
Maadhimisho haya hayakuja ghafla bali ni matokeo ya mchango wa wasomi wengi, wanaharakati na watafiti walioandaa kwa moyo wao wa dhati maandishi, kujenga hoja na kuonesha ushahidi kuwa Kiswahili sasa si cha Tanzania tu, bali lugha ya Kiafrika ilienea duniani kote.
Siku hiyo huadhimishwa katika vyuo vikuu na mashirika mbalimbali kupitia maonesho ya kitamaduni ikiwemo ngoma, muziki kwa Kiswahili na mapishi ya kitamaduni.
Wataalamu wa lugha ya Kiswahili pia walishiriki katika majadiliano na mazungumzo ili kuboresha lugha na kutoa mwanga juu ya mustakabali wa lugha hiyo katika siku zijazo.
Zanzibar pia ilishiriki Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani, wakati Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Polisi Zaywani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja ambapo alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Wakati watu wa Kisiwa cha Lamu nchini Kenya hawakuachwa nyuma, wakisherehekea siku hiyo kwa nyimbo, mashairi na maonesho mbalimbali.