«Ghazaly» ni Mzungumzaji katika jukwaa la kimataifa la watafiti na wanafunzi wa Chad kwenye Jamhuri ya Kiarabu ya Misri
«Hassan Ghazaly», Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, alishiriki katika mkutano wa mazungumzo ulioitwa “Mahusiano ya Misri na Chad” kupitia jukwaa la kimataifa la watafiti na wanafunzi wa Chad kwenye Jamhuri ya Kiarabu ya Misri katika toleo lake la kwanza, linalofanyika mnamo siku za Jumanne na Jumatano, Desemba hii tarehe 6 na 7, kwa kushirikiana na kampuni ya Makandarasi wa Kiarabu, pamoja na Ufadhili wa Ubalozi wa Jamhuri ya Chad nchini Misri, kwa mahudhurio ya viongozi wa kampuni ya Makandarasi wa Kiarabu na wanachama kadhaa wa Ubalozi wa Chad, na kundi la maprofesa, watafiti, wataalamu wa kitaaluma na wanafunzi wageni na wahusika wa utafiti wa kisayansi.

Mwanzoni mwa hotuba yake, «Ghazaly» alielezea furaha yake kubwa kwa ushindi wa wanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Chad kwa uenyekiti wa Kamati ya Rasilimali watu ya baraza la kijamii na kiuchumi la Umoja wa Afrika kwa miaka minne ijayo, akiashiria mchango mkubwa wa wanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Chad katika nyanja za mafunzo na uwezeshaji, juhudi zao katika kukuza mshikamano wa amani na utulivu wa kitaifa na kikanda, na maarufu zaidi miongoni mwake ni mafunzo ya vijana wa kiume na wa kike 1800, katika majimbo 6 ikiwa ni pamoja na: “wadi Absha”, shari ya katikati “Sar”, Jiwe la lamis “Musacet” na bathaa “Mama wa Mawe” pamoja na mji mkuu N’djamena, lililosifiwa moja kwa moja kutoka kwa mheshimiwa Rais “Mohamed Idriss Deby” Rais wa Jamhuri ya Chad.

«Ghazaly» aliendelea akisisitizia michango ya vijana wa Harakati ya Nasser ya Kimataifa kwa vijana huko Chad katika nyanja mbalimbali na mikutano yao mingi ya uratibu na viongozi watendaji na watoa maamuzi katika ngazi ya kitaifa kulingana na jukumu lililotolewa na Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika kuwajulisha yanayohusu uzoefu wa Misri katika kujenga taasisi za kitaifa, pamoja na kutoa mikutano kati ya ujumbe wa Chad na watunga maamuzi wa Misri, na ambao maarufu zaidi ulikuwa mkutano wa ujumbe wa Chad na Dkt. Mohammed Shaker, Waziri wa Umeme na Nishati wa Misri ndani ya shughuli za Udhamini.

«Ghazaly» aliongeza kuwa wakati wa kuchangia kusaidia njia za ushirikiano wa nchi mbili kati ya Misri na Chad, tulifanikiwa kuratibu kutia saini kwa itifaki ya ushirikiano kati ya Benki ya Chakula ya Misri na Benki ya Chakula ya Chad, na mkusanyiko wa benki za chakula za mkoa, pamoja na mshikamano wa vijana wa Harakati ya Nasser nchini Chad na wajasiriamali na wafanyabiashara wa Misri wakati wa uwepo wao nchini Misri kando ya ushiriki wao katika mkutano wa hali ya hewa wa COP27.

Alihitimisha akisema kuwa juhudi za Harakati ya Nasser kwa Vijana huko Chad, haswa katika mfumo wa vijana na wanawake, na kupambana na ufisadi zimepata tuzo na heshima kadhaa kitaifa na kimataifa, maarufu zaidi ni; wanachama wawili wa Harakati hiyo ni "Yusra Diay" amepata cheo cha Mpandaji, "Sharaf El-Din Nasr Tedio" na cheo cha kiongozi katika mfumo wa vijana kwa ishara ya ufanisi katika medali ya ustahili wa kiraia kutoka kwa Mheshimiwa Rais “Mohamed Idriss Deby” kwa mujibu wa amri namba 385 mnamo Septemba 2021, mbali na ushindi wa «Mohamed Lary», mwanachama wa Harakati ya Nasser nchini Chad kwa tuzo ya uadilifu na kupambana na rushwa kutoka kwa kundi la Chad nchini Marekani, akisisitiza kuwa hii ilikuwa mara ya kwanza ambapo tuzo hiyo kutolewa kwa mwanaharakati wa kitaifa.

Ikumbukwe kuwa Jukwaa la kimataifa la watafiti na wanafunzi wa Chad lilianzishwa mnamo 2003 na wanafunzi na watafiti nchini Chad, wakijaribu kujenga jukwaa kwa ajili ya mawasiliano, kubadilishana mawazo, majaribio na uzoefu kupitia njia zinazoruhusu kushiriki kwa mtafiti na mwanafunzi wa Chad katika ngazi ya kitaifa na kimataifa ili kuongeza jukumu lake katika maendeleo ya nchi yake, na kujadili masuala ambayo Chad inayopambana nayo, na kuchangia katika kuweka masuluhisho sahihi katika mfumo wa matokeo na mapendekezo yaliyotolewa na watafiti mwishoni mwa jukwaa na kuwasilishwa kwa watoa maamuzi na mamlaka husika.
