Ubalozi wa Jamhuri ya Armenia Mjini Kairo wakaribisha Mhitimu wa kwanza Armenia kutoka Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Ubalozi wa Jamhuri ya Armenia Mjini Kairo wakaribisha Mhitimu wa kwanza Armenia kutoka Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Imetafsiriwa na: Al-Sayeda Tarek 
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr 

Balozi Hrachia Boldian alimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Armenia katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Hakob Makdis na Tsovinar Sargsyan, washiriki wa kwanza wa Armenia katika toleo la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, uliofanyika chini ya ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, na ambapo viongozi wa vijana wa 150 kutoka nchi zisizo na uhusiano na za kirafiki walishiriki, wakati wa kipindi cha Mei 31 hadi Juni 17, 2022, katika Nyumba ya Mamlaka ya Uhandisi huko Kairo.

Wakati wa mkutano huo, Balozi Hrachya Boldian alijadili na wahitimu matarajio ya ushirikiano wa kiuchumi wa Armenia na Misri, pamoja na jukumu la vijana wa Armenia katika kuimarisha mahusiano ya kiuchumi kati ya Armenia na nchi za Kiarabu.

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni  matokeo kwa juhudi za muda mrefu za Misri zinazolenga kuchochea elimu na maendeleo ya vijana wanchi zisizofungamana na upande wowote na za kirafiki na kupata nafasi za uongozi katika nafasi za kufanya maamuzi, ni muhimu kutambua kuwa mpango huo hutoa fursa kwa vijana kutoka duniani kote kupata "mahusiano ya kazi" ambayo hutumika kama msingi thabiti wa msaada wa pamoja na uelewa wa pamoja katika siku zijazo, na Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa pia inalenga juhudi za kufikia Malengo ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa na ushirikiano wa Kusini-Kusini.

Katika hotuba yao, wahitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wanaangazia masomo yaliyofanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, Seti za Seneti, Ofisi ya Waziri Mkuu, Chuo cha Polisi, na miundo kadhaa yenye thamani  imeyoleta thamani kubwa katika kuchangia maendeleo ya viongozi wa vijana.