Mhitimu wa Udhamini wa Nasser ni mzungumzaji katika Kongamano la kitaifa la"Uhalisia wa Ushiriki wa Vijana wa Tunisia katika Maamuzi"

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser ni mzungumzaji katika Kongamano la kitaifa la"Uhalisia wa Ushiriki wa Vijana wa Tunisia katika Maamuzi"

Kwa Usimamizi wa Chuo cha Kiarabu ya Haki za Kibinadamu na kwa mwaliko wa Kundi la Kimataifa la Basma la Misaada ya Kibinadamu, Yassin Fattahly, Mhitimu wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alishiriki katika Kongamano la kitaifa lililofanyika Februari 8,2022, mjini Tunisia, kwa anwani ya "Uhalisia wa Ushiriki wa Vijana wa Tunisia katika Maamuzi".

Kongamano hilo linazingatiwa kama fursa ya kuangazia uhalisia wa jukumu la vijana katika kushiriki katika vituo vya maamuzi nchini Tunisia, na kuonesha mazoea chanya katika uwanja huo, na changamoto zinazowakabili vijana katika kushiriki katika masuala ya kisiasa, ambapo warsha ni hatua ya kuanzia ili kuwezesha vijana wa Tunisia kushiriki katika kufikiri kwa kupitia kupata masuluhisho ya ufanisi na endelevu.

Na hiyo inafanywa kwa kusikiliza ushahidi wa wawakilishi wa vijana kutoka maeneo na mamlaka mbalimbali (Vyama, Jumuiya, Mipango huru, Tovuti za mitandao ya kijamii), na kuunda vikundi vya kuzingatia uhusiano wa vijana pamoja na taasisi rasmi.