Wiki ya Anga za Juu Duniani

Imetafsiriwa na/ Abdelmenem Khalefa
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed
Mwanza wa Wiki ya Anga za Juu Duniani huambatana na maadhimisho ya uzinduzi wa satelaiti ya kwanza mnamo tarehe Oktoba 4, 1957 kwenda anga za juu, ikitangaza mwanzo wa utafutaji wa anga za juu, wakati mwisho wa wiki ya anga za juu mnamo tarehe Oktoba 10 huambatana na kuingia kwa nguvu ya Mkataba wa "Carta Magna" mnamo Oktoba 10, 1967, ambayo ni Mkataba wa Kanuni zinazoongoza Shughuli za Mataifa katika uwanja wa uchunguzi wa nafasi na matumizi ya anga za juu, ikiwa ni pamoja na Mwezi na miili mingine ya mbinguni.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliidhinisha Wiki ya Anga za Juu Duniani kwa kusherehekea mchango wa sayansi na teknolojia ya anga za juu katika kuboresha maisha ya binadamu wote, kwa azimio Na. 54/68 la tarehe Desemba 6, 1999, mradi tu mandhari ya umoja huchaguliwa kila mwaka katika ngazi ya kimataifa, kwa lengo la kukuza ushirikiano wa kimataifa katika kukuza ufahamu na kuelimisha umma kuhusu shughuli za anga za juu.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy