Siku ya Dunia ya Urithi wa Sauti na Kuona "Audiovisual"

Siku ya Dunia ya Urithi wa Sauti na Kuona "Audiovisual"

Imetafsiriwa na/ Husna Mohammed 
Imeharirwa na/ Mervat Sakr 

Vifaa vya sauti na maandishi vinawakilisha dirisha Ulimwenguni linalochangia Uelewa wetu wa Ulimwengu tunaoshiriki, unathibitisha kumbukumbu yetu ya pamoja, na huunda hadithi tunazofurahiya na kuongoza zamani zetu, na urithi wa sauti unahusiana na haki ya msingi ya binadamu, ambayo ni Uhuru wa mtiririko wa mawazo na mzunguko wao wa bure kupitia neno na picha, na pia inaweza na kwa kweli kujenga amani katika akili za wanadamu, na kujenga vifungo vya Uhusiano na Urafiki kati yao. 

Katika Mkutano Mkuu wa 2005, UNESCO, kwa azimio la 53/33, ilitangaza 27 Oktoba kama Siku ya Dunia ya Urithi wa Sauti na Kuona "Audiovisual", ikiambatana na maadhimisho ya kupitishwa na Mkutano Mkuu katika kikao chake cha ishirini na moja, katika 1980, ya Pendekezo la Ulinzi na Uhifadhi wa Picha za Kusonga.

Maktaba ya Umoja wa Mataifa ya Sauti na Kuona "Audiovisual" ina zaidi ya maudhui ya kihistoria ya 6,330 pamoja na video 49,400 zilizorekodiwa, na wanaakiolojia katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa hufanya kazi saa nzima kuhifadhi rekodi karibu elfu 40.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy