Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni mshiriki katika Programu ya Ubunifu wa Kijamii na Teknolojia INSAF / FAM
Imetafsiriwa na: Shams Adel
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Manal Ben Ammar, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kwa kikundi cha pili, alishiriki katika mpango wa "Insaf / FAM" kwa uvumbuzi wa kijamii na teknolojia kwa ajira bora ya wanawake wa Tunisia kwa mwaka 2020-2030, ambayo hufanyika chini ya kauli mbiu "Ujenzi wa Uwezo katika Elimu ya Juu" kwa msaada na ufadhili wa Umoja wa Ulaya. Mpango huu uko ndani ya muktadha wa uundaji wa miradi ya maendeleo baada ya mafunzo na Kihispania "Chuo Kikuu cha Cadés" kwa kushirikiana na vyuo vikuu vya Kituruki na Tunisia kama vile Chuo Kikuu cha Monastir, Chuo Kikuu cha Sfax, Chuo Kikuu cha Kairouan, na Chuo Kikuu cha Gabes.
Ni muhimu kutambua kwamba "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa " unalenga kujenga kizazi kipya cha viongozi wa mabadiliko ya vijana na maono kulingana na mwelekeo wa urais wa Misri katika nchi mbalimbali kupitia ushirikiano, pamoja na kuunganisha viongozi wa vijana wenye ushawishi mkubwa duniani na mafunzo, ujuzi muhimu na maono ya kimkakati.