"Nesrin  Alsabahi" mjumbe wa mradi wa Umoja wa Bonde la Mto Nile ashinda tuzo ya Helmi Shaarawi

"Nesrin  Alsabahi" mjumbe wa mradi wa Umoja wa Bonde la Mto Nile ashinda tuzo ya Helmi Shaarawi
"Nesrin  Alsabahi" mjumbe wa mradi wa Umoja wa Bonde la Mto Nile ashinda tuzo ya Helmi Shaarawi
"Nesrin  Alsabahi" mjumbe wa mradi wa Umoja wa Bonde la Mto Nile ashinda tuzo ya Helmi Shaarawi

Nesrin Alsabahi mtafiti, mjumbe wa timu ya utafiti kwenye mradi wa " Umoja wa Bonde la Mto Nile.... Mitazamo ya baadaye" na mtafiti mhusika kwenye mambo ya Kiafrika kwenye kituo cha kimisri cha mawazo na masomo ya kimkakati (ECSS) alishinda tuzo ya mtafakari mkuu Helmi Shaarawi " mlinzi wa Tamaduni za Kiafrika" kwa masomo ya Kiafrika mnamo mwaka (2020-2022), ambapo utoaji wa tuzo kwa mshindi siku ya jumatatu mwezi huu wa Oktoba kwenye Maktaba kuu ya Misri.

Alsabahi alipata shahada ya sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Beni Suef mnamo 2017 kwa daraja zuri sana lenye heshima, ameshaathiri kwa utafiti na tafiti zilizochapishwa ili kuzingatia masuala ya ugaidi, migogoro, mabadiliko ya hali ya hewa na eneo la Sahel la Afrika Magharibi kwenye suala la  masomo ya kiafrika kupitia miaka mitano baada ya kuhitimu kwake,  alishiriki kama mzungumzaji wa warsha " mustakabali wa Afrika ulimwenguni baada ya janga la uviko kwenye Ajenda ya Kiafrika 2063" katika Kongamano la Vijana la mwaka wa 2021, alieleza kuonesha majaribio ya nchi za Kiafrika kwenye kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa :
utafiti wa hali ya kimisri, kisha mwaka huu alikamilisha shahada ya Uzamili katika masomo ya Kiafrika, chuo kikuu cha Kairo Kwa ubora, na hivi karibuni amekuwa mtafiti  wa Uzamivu katika masomo ya Kiafrika katika kitivo cha masomo ya kuhitimu Afrika, Chuo Kikuu cha Kairo.

Kwa upande wake Alsabahi alielezea hisia yake alipopokea habari ya kushinda kwa tuzo ya mwalimu Helmi Shaarawi, akiisifu habari hii kama afadhali habari kuliko zote kwake kutokana na Kiwango cha juu cha tuzo katika duru za Kiafrika, akielezea jinsi anavyojivunia kuchagua tasnifu ya bwana wake mwenye mtafakari mkuu huyu katika masuala ya masomo ya kiafrika alivyochaguliwa kama Utafiti bora katika masuala ya Afrika katika Utafiti Bora kuliko wote katika Masuala ya Afrika mnamo 2022.

Na katika muktadha huo huo, tasnifu yake inajumuisha sehemu ya utangulizi, sura tatu na mada ya mwisho "hitimisho".

mtafiti alielezea athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye migogoro ya ndani katika nchi za Afrika Mashariki, ambapo sehemu ya utangulizi yajumuisha mwenendo wa kinadharia katika utafiti wa uhusiano kati ya mabadiliko ya hali ya hewa na migogoro ya ndani , ama sehemu ya kwanza yazungumzia hali ya mabadiliko ya tabianchi kwenye Afrika Mashariki, na kwenya sehemu ya pili, mtafiti alijadili athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika mzizi na maendeleo ya migogoro ya ndani Afrika Mashariki, katika sehemu ya tatu alielezea sera za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na Jukumu lake katika kudhibiti migogoro ya ndani kwenye Afrika, ama mada ya mwisho inajumuisha matarajio ya kujenga amani ya mazingira Barani Afrika.


Na kwa upande wake, Hassan Ghazali mwanzilishi wa mradi huo na mjumbe wa timu ya utafiti kwenye kikundi cha " Afrikianion" alieleza kuwa mtafiti Nesrin Alsabahi mojawapo ya watafiti waliibuka katika umoja wa utafiti wa mradi, akazingatia kuwa alishiriki kwenye matukio mengi kwa namna ya pekee miongoni mwa matukio haya yalikuwa mkutano wa kwanza kwa vijana wa kimisri na Sudan, miongoni mwa "mradi wa Umoja wa Bonde la Mto Nile... Mitazamo ya baadaye" pamoja na ushiriki wa kama mtafiti katika maandalizi ya kwanza kwa shuleya Kiafrika 2063 mnamo mwaka 2018, akasisitiza umuhimu wa kuiga namna ya tuzo na matukio haya haswa kwenye suala la masomo ya kiafrika yanayoendelea kwa sababu ya kuimarisha na kuhimiza ushiriki wa vijana wengi miongoni mwa vijana watafiti ili kutajirika suala hilo imehitaji bado masomo kadha na uzalishaji wa kiakili unaotokana na Waafrika wenyewe.

Ishara inaangazia kuwa mtafakari mkuu Helmi Shaarawi alikuwa na Michango mingi kwenye suala la Kiafrika, miongoni mwa anasimamia faili ya harakati za ukombozi wa Afrika nchini Misri kupitia kipindi cha rais wa Jamhuri wa zamani Gamal Abdel Nasser, alifanya kazi pia kama mwalimu wa sayansi ya kisasa kwenye chuo kikuu cha Goba kwenye Sudan (1981- 1982) na mtaalamu katika mahusiano ya kiarabu ya kiafrika kwenye taasisi ya kiarabu kwa elimu, utamaduni na sayansi nchini Tunisia (1982-1986).
Na pia alikuwa Rais wa zamani sana kwa Jumuiya ya kiafrika kwa sayansi ya kisasa, na mwanzilishi wa kituo cha utafiti wa Kiarabu na kiafrika, alizindua tuzo hii kwa mara ya kwanza  mnamo mwaka wa 2010, kama tuzo ya mwaka iliyokadiriwa kwa paundi maelfu 10 inapewa kwa utafiti bora wa kisayansi katika masomo ya Kiafrika, na  sharti la tuzo hiyo linatakiwa kuiandaa kwa ajili ya kuchapishwa na kuiwasilisha katika sherehe maalumu pale kitabu kitakapotolewa na kukabidhi cheti cha shukrani na kiasi kidogo cha pesa kwa mtafiti.