Mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana " Bening" ashinda nafasi ya Katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa Afrika
(Kwa Hamasa na Jitihada, tunafanya ndoto iwe hai na kuinua juu bendera za taifa na Bara letu), Hiyo ni falsafa ya kiongozi kijana wa Ghana " Ahmed Bening" aliyeshinda nafasi ya Katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa Afrika baada ya mahudhurio yake na ushawishi wake mkubwa, na juhudi zake mnamo kipindi kilichopita katika Umoja kuanzia 2017 hadi 2021 kama Naibu wa Katibu mkuu, ambapo alikuwa akifanya kazi kati ya Vijana Barani Afrika na alifanya kazi kupitia shughuli zake nyingi kupanua upande wa ushirikiano na ushiriki wa Vijana unaotegemea Umoja kamili wa Vijana, nguvu na wa kudumu, ili kufufua harakati ya Umoja wa Afrika na kuendeleza Vijana wake kwa mujibu wa Maoni ya 2030 na Ajenda ya Afrika 2063; kufanya Afrika kamili, iliyoendelea, na lenye ustawi kama tunavyotaka.
Bening alihitimu masomo kutoka kwa Chuo Kikuu cha mafunzo ya maendeleo " Tamale" , huko Ghana na alifanya kazi wakati wa masomo yake kama Katibu wa Umoja wa kitaifa wa wanafunzi wa Ghana, na baada ya uhitimu wake alifanya kazi katika Shirika la kimataifa liandaalo tamasha za vijana na wanafunzi wa Afrika kusini za kimataifa mnamo 2010, Ekuador mnamo 2013 na Urusi mnamo 2017, Na pia ni mwanachama wa baraza la uongozi wa jukwaa la vijana wa "Brics" huko Afrika kusini, na Mwenyekiti wa baraza la Almostakbal nchini Ghana, pamoja na alishika nafasi ya Katibu mkuu wa Shirika la Vijana wa Afrika magharibi kati ya 2013 na 2015, na pia Naibu wa kamishna na mkurugenzi wa mipango ya Umoja wa wanafunzi wa Afrika.
Bening alipata tuzo kadhaa; kutokana na juhudi zake Barani kwa kuwawezesha Vijana, Kuwasilisha sauti zao,kukuta nafasi za kazi, Ushirikiano na kuimarisha njia za Ushirikiano kati yao kwa kitaifa na kimataifa, ikiwemo tuzo ya vijana wa Afrika ambayo yenye ushawishi mkubwa zaidi kutoka tuzo za Afro_ Arab kama Mwanaghana wa kwanza aliyepokea tuzo hiyo kutoka baraza la kiarabu la Afrika, Na inatajwa kuwa alipopokea hiyo aliwazawadia vijana wote ambao ni wahanga wa hali ngumu, alijiahidi kuwa kuitoa kwa vijana wote katika jamii zilizonyimwa na kuhitaji zaidi, akisisitiza kuwa kila kitu inawezekana pia kwa juhudi tunaweza kuhifadhi ndoto kuwa hai, Na pia kiongozi huyo mpendwa alishinda tuzo ya Vijana wenye ushawishi mkubwa mnamo 2018 kutoka tuzo za Vijana washauri wenye mafanikio katika eneo la juu la kikanda la magharibi Barani Afrika.