Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni msimamizi wa mfano wa Bunge la Moroko

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni msimamizi wa mfano wa Bunge la Moroko

Imetafsiriwa na: Omar Sherif
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr 

Dkt. Hamza Awahd, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na Mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Moroko, anasimamia mfano wa simulizi ya Bunge la Moroko katika toleo lake la tatu chini ya kauli mbiu "Vijana na Demokrasia", imeyoandaliwa na Chama cha Uamsho wa Vijana na Shirika ya Ujerumani "Konrad Adenauer", na kwa sasa inafanyika Casablanca kutoka Januari 24 hadi 30, 2022, na mpango huo umepangwa kujumuisha simulizi ya Haki, Sheria, na Kamati ya Haki za Binadamu kwa Kiarabu, pamoja na simulation ya Kamati ya Mambo ya Ndani kwa Kifaransa, kuhusu mada ya "kutoa pasipoti ya chanjo" na "dharura ya afya" kwa mtiririko huo. 

Kwa upande wake, Mohadi alisema kuwa mtindo wa uigaji wa bunge la Moroko una lengo la kuongeza ushiriki wa vijana na kuwajumuisha katika kazi za kisiasa za Moroko, kwa kuwawezesha kuelewa utaratibu wa kazi za kamati za sheria, kuzingatia majukumu ya bunge katika sheria na kutunga sheria, akibainisha kuwa kikao hiki pia kitajumuisha kuiga mchakato wa uchaguzi. 

Katika muktadha unaohusiana, Mohidi alisisitiza kuwa kuiga kamati za bunge na uchaguzi ni fursa nzuri kwa washiriki kutoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali kwenye eneo la Moroko, hasa kuhusiana na hali ya mchakato wa uchaguzi huko. 

Kwa upande wake, Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, alipongeza juhudi za wanachama na waratibu wa Harakati ya Nasser katika Ufalme wa Moroko, akieleza kuwa hii ni muktadha sahihi ambao Harakati hiyo imekuwa ikilenga tangu kuzinduliwa kwake, kwa kiasi kikubwa inayolenga kuunda kiongozi kijana na kiongozi mwenye mafanikio, ambapo harakati hiyo tayari imefanikiwa, na labda udhihirisho wake maarufu ni uteuzi wa Dkt. Mohamed Nofal kama mshauri wa kisheria kwa Waziri wa Maji nchini Moroko mnamo tarehe Novemba 2021, pamoja na matukio ya ufahamu na majadiliano yanayohusiana na masuala ya kisiasa ya Moroko yaliyozinduliwa na harakati, ikiwa ni pamoja na Jopo la majadiliano kuhusu jukumu la vijana na wanawake katika uchaguzi wa 2021 nchini Moroko. 
 
Ghazaly alihitimisha kwa kuonesha jukumu muhimu lililochezwa na mifano ya simulizi katika uwanja wa makada wa vijana wenye sifa kwa uongozi, kuchukua jukumu, na kuimarisha ujuzi wao wa karibu wa mbinu za kufanya maamuzi ndani ya miundo ya taasisi za kitaifa na kimataifa, akisisitiza kuwa Misri ina historia ndefu na uzoefu mzuri na mifano ya simulizi, na hata mifano ya simulizi ni mojawapo ya matukio muhimu zaidi ya vijana ambayo serikali ya Misri inalipa kipaumbele kikubwa, kwa mfano, mfano wa simulation wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa "UNHRC", Rais Abd Rais El-Fattah El-Sisi, aliyekuwa mmoja wa matukio makuu ya Jukwaa la Vijana Duniani 2022.