Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa akutana na Mkurugenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa akutana na Mkurugenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mkurugenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Ray Keleo alimpokea Mhitimu wa Kundi la Tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Mansuza Kengo katika makao makuu ya ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri huko Dodoma, mji mkuu wa Tanzania.

Mkutano huo ulishughulikia kufahamiana na Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, pia kujadili na kuchunguza uwezekano wa kuanzisha na kutekeleza mpango wa kubadilishana kati ya vijana wamisri na watanzania mnamo kipindi kijacho. Na kwa upande wake, Bw.Ray Keleo alisisitizia umuhimu wa ushirikiano wa pamoja kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, na nia ya Tanzania katika kuendeleza na kujali nchi yake katika kuongeza msaada wa kiufundi unaotolewa na Misri kwa makada wa Tanzania katika nyanja za kuwajengea uwezo, elimu, vijana na michezo, haswa kwa kuzingatia mpango kabambe wa maendeleo ambao Tanzania inataka kuutekeleza.

Na Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri iliandaa matukio ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa ushiriki wa viongozi vijana 150 kutoka nchi zisizofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki, mnamo kipindi cha kuanzia Mei 31 hadi Juni 17, mwaka wa 2022 katika Jumba la Mamlaka ya Uhandisi mjini Kairo.

Na Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuhamisha uzoefu mkale wa Misri katika kuunganisha na kujenga taasisi za kitaifa, licha ya kuunda kizazi cha viongozi  vijana kutoka nchi zisizofungamana zenye maoni sambamba na ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza mwamko wa jukumu la Harakati ya kutofungamana la kihistoria na jukumu lake mnamo siku zijazo, pamoja na kuamsha jukumu la k vijana wa nchi wanachama wa Jumuiya ya NYM isiyofungamana, na kuunganisha viongozi vijana wenye ushawishi mkubwa katika ngazi ya nchi zisizofungamana na nchi rafiki.

Pamoja na kutoa fursa sawa kwa jinsia mbili, kama ilivyoashiriwa na lengo la tano la Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, pia, unawawezesha vijana na kuwapa fursa kwa watendaji wa nchi mbalimbali Duniani ili kushirikiana pamoja  na kufanya mashirikiano katika nyanja mbalimbali, si tu Barani, bali ya kimataifa, kama inavyoashiriwa na lengo la kumi na saba la malengo ya Maendeleo Endelevu.