Kumtukuza Mjumbe wa Harakati ya Nasser kwa Vijana kwa tuzo ya mwanahabari mshawishi bora zaidi kwa huduma ya jamii kwa mwaka wa 2022

Shirikisho la Vijana la Afro-Asian la sinema mpya lilimtukuza mwanahabari Sharif Hassan, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na Mjumbe wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, kama mwanahabari bora zaidi anayelenga kuhudumia jamii, na kumchagua miongoni mwa orodha ya Watu 100 wenye ushawishi bora zaidi ulimwenguni mwa Kiarabu kwa mwaka wa 2022, ambapo hii ilitokea mnamo wa tamasha la tisa la kila mwaka lililoanza Ijumaa jioni, tarehe 30 Dec kutoka mwezi huu, lililoandaliwa na Umoja kwa ushirikiano na akademia ya kimataifa mustakabali wa Misri kwa somo la utu na Amani, Umoja wa Kitaifa wa Kupambana na Ugaidi na Ufisadi, na Gazeti la Siasa la Kimataifa pamoja na Ufadhili wa Mtukufu Princess Sheikha Intisar Al-Sabah.
Mwanahabari huyo, Sherif Hassan, alielezea furaha yake kwa kutunukiwa heshima hiyo, akiashiria nafasi ya kiutamaduni inayotekelezwa na tamasha hilo kila mwaka katika maeneo ya Kiarabu, akiashiria haja ya kufanyika matukio kama hayo ili kuimarisha nafasi ya utamaduni, sanaa na amani katika jamii, akisisitiza uungaji mkono wake kama mwandishi wa habari kwa shughuli hizi kwa kumulika katika vipindi vyake mbalimbali.
Ikumbukwe kuwa Harakati ya Nasser kwa Vijana inazingatiwa kama mfumo wa maendeleo uliozinduliwa katika mwezi wa Julai, mwaka wa 2019, ambapo katika miaka michache, iliweza kuunda jukwaa la mahusiano mapya na endelevu ya vijana yenye sifa za maadili ya juu, mshikamano, na kutofuatana. Na pia harakati, kupitia waratibu wake, imehakikisha ushawishi mkubwa katika takriban nchi 65 hadi sasa katika mabara manne, Asia, Afrika, Amerika ya Kusini na Australia, ambapo kila mmoja wao alifanya kazi, ndani ya uwanja wa ushawishi wake, uwezo wa nchi yake, na kulingana na matakwa ya jamii yake, na walianzisha programu nyingi za maendeleo katika uwanja wa kuwarekebisha na kuwawezesha vijana.