Harakati ya Nasser kwa Vijana yafanya kikao cha mashauriano ya vijana Mauritania
Imetafsiriwa na: Nadia Mahmoud
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Ndani ya muktadha wa mpango wa kuamsha kazi ya vijana kwa mkoa wa Afrika Kaskazini na ndani ya muktadha wa kuratibu juhudi zinazoambatana na kufikia ushirikiano kati ya vijana wa kaskazini mwa bara, mkutano wa maandalizi utafanyika kati ya ofisi ya kikanda ya Harakati ya Nasser kwa Vijana huko Kairo na vijana wa Mauritania, na mkutano utafanyika saa kumi jioni Kairo na saa nane za Nouakchott.
Vijana wa Mauritania tu wanapaswa kuacha maoni (jina - nchi - taasisi) ili kuwatumia kiungo kwenye mkutano.
Mkutano kwa lugha ya Kiarabu, ambayo ni lugha rasmi ya nchi za Kaskazini mwa Afrika katika Umoja wa Afrika.