Mshikamano wa Kimataifa wajadili mifano maarufu ya Afrika kwenye kilimo
Uzoefu wa Tanzania katika kilimo uko kwenye Meza ya Mpango wa Mshikamano wa Kimataifa
Ndani ya mfululizo wa vipindi vya kipindi cha Mazungumzo wa Mshikamano wa Kimataifa (Idara ya Kiswahili), Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa liliandaa mjadala wenye mada: Mageuzi ya Kilimo: “Uzoefu wa Misri na Tanzania katika Kukabiliana na Changamoto na Mafanikio,” Sambamba na Siku ya Wakulima wa Tanzania.
Kipindi hicho kilihudhuriwa na Bwana Thomas Amas Mtchiwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Stadi za Maisha (ALSF) Mabuibande, Dar es Salaam, Tanzania, Mtaalamu wa masuala ya ulinzi wa mazingira na kuwajengea uwezo vijana, pamoja na kundi la wasomi na watafiti katika lugha na masuala ya Afrika.
Thomas Mchiwa amefungua kipindi hicho kwa kuangazia maendeleo ya kilimo nchini Tanzania, akieleza athari zake kubwa kwa jamii ya eneo hilo, na aligusia wakati wa hotuba yake changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo, kama vile matatizo ya upatikanaji wa mazao na hali ya ardhi inayoathiri tija kwa wakulima, akielekeza kuhama kutoka kwa zana za kilimo za jadi, zimezokuwa kikwazo kwa wakulima, kutumia mbinu za kisasa za umwagiliaji zinazochangia kuboresha uzalishaji, akisisitiza umuhimu wa ufadhili kwa kusaidia wakulima katika kutumia mbinu hizi na kuwekeza kwenye zana za kisasa za kilimo.
Mchiwa alipitia jukumu la serikali na taasisi katika kusaidia sekta ya kilimo kwa kutoa misaada inayohitajika na kutoa programu za mafunzo zenye lengo la kuboresha ujuzi wa wakulima na kuongeza ufanisi wao, akaeleza umuhimu wa kuzingatia ubora wa mazao katika kufikia usalama wa chakula na kuchangia uchumi wa taifa kupitia usafirishaji wa mazao ya biashara kama kahawa na chai, akizungumzia ziara ya Rais Mama Samia mkoani Morogoro, ambapo alisikiliza kero za wakulima kuhusu bei kubwa na uhaba wa mazao, akisisitiza dhamira ya serikali ya Tanzania kutoa msaada unaohitajika ili kuimarisha sekta hiyo.
Kipindi hicho kilisimamiwa na Mtafiti Yasmine Kamal, na wakati wa mazungumzo yake alijadili historia ya uzoefu wa Misri katika uwanja wa kilimo na alirejelea sheria ya umiliki wa ardhi iliyokuwa ikitumika wakati wa Ukoloni wa Uingereza nchini Misri, ambayo ilizuia umiliki wa ardhi za kilimo kwa umma kwa ujumla, kwani ziliwekwa kwa kundi maalumu la wamiliki, akielezea jinsi Mapinduzi ya Julai 1952 yalifanikiwa kumaliza muongo huo, akiashiria Sheria ya Mageuzi ya Kilimo iliyoletwa na Rais Gamal Abdel Nasser, iliyofuta mfumo wa kimwinyi na usambazaji wa ardhi kwa wakulima, na kuwapa wamiliki wa ardhi fursa ya kumiliki ardhi ya kilimo.
Kwa upande wake, Mwanaanthropolojia Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa, alieleza kuwa uzoefu wa Misri na Tanzania katika nyanja ya kilimo hutoa mifano maarufu ya mageuzi ya kilimo barani Afrika, na akisifu njia maarufu iliyochukuliwa na Tanzania kupitia mipango ya kitaifa kama vile "Klimo Kwanza", iliyochangia kuboresha usalama wa chakula na maendeleo ya kiuchumi katika maeneo ya vijijini.
Ghazaly aliongeza kuwa ndani ya muktadha wa sera ya kujifunza ya Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa, tulikuwa na nia ya kutoa fursa kwa wawakilishi wa Idara ya Lugha ya Kiswahili ya Mtandao kuwasilisha karatasi zao za utafiti wakati wa kipindi kwa njia shirikishi kuhusu uzoefu wa kuongoza Misri ya Tanzania katika uwanja wa kilimo, iliyoshughulikia mambo kadhaa, hasa: Ulinganisho kati ya Siku ya Mkulima nchini Misri na Siku ya Wakulima nchini Tanzania, nyingine inayoshughulika na historia ya Siku ya Wakulima nchini Tanzania, na karatasi yenye kichwa "Siku ya Wakulima: Hali halisi ya kilimo kati ya changamoto na fursa", nyingine yenye kichwa cha habari "Mwelekeo wa utamaduni wa Siku ya Wakulima (NaneNane) nchini Tanzania", kauli mbiu "Udongo ni chanzo cha uhai", na nyingine ni "Siku ya NaneNane ni Siku ya Mavuno ya Matumaini nchini Tanzania".
Ghazaly aliongeza kuwa uongozi wa uzoefu wa Misri ni wa zamani kama historia katika nyanja ya kilimo, lakini ulipata mwelekeo mzuri wakati wa enzi za kiongozi wa zamani Gamal Abdel Nasser, na hivi karibuni wakati wa enzi za Rais Abdel Fattah Al-Sisi kupitia miradi mikubwa ya kitaifa kama vile Mradi wa Delta Mpya, na mpango wa kuhamia kilimo cha digital, akisisitiza kuwa uzoefu huu unaonesha wazi jinsi mageuzi ya kilimo yanaweza kuchangia kufikia maendeleo endelevu na kuimarisha usalama wa chakula katika bara la Afrika, hasa kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi.
Ni vyema kutambua kwamba Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa ni wa hiari na usio wa faida, na programu zake hutolewa bila malipo kabisa na hupangwa kwa juhudi binafsi bila kupokea msaada wowote wa kifedha. Mpango wa Mazungumzo wa Mshikamano wa Kimataifa pia huzindua vikao vya majadiliano katika lugha mbalimbali: Kiarabu/Kihispania/Kiswahili/Kifaransa, Kiingereza, na Kirusi, kama jukwaa wazi la majadiliano na kubadilishana kiakili kuhusu masuala ya kawaida ya kitamaduni, kwa lengo la kukuza mshikamano kati ya watu kutoka tamaduni na asili tofauti duniani kote, pamoja na utaratibu muhimu ambao huwapa vijana wa Misri na wanafunzi kusoma lugha fursa ya kufanya mazoezi ya lugha yao ya kujifunza na watu wa asili katika Asia, Ulaya, Afrika na Amerika ya Kusini, ili kuandaa makada na viongozi wenye uwezo wa kuelewa mabadiliko yanayotokea duniani.