Harakati ya Nasser kwa Vijana yatoa maombolezo kwa Mtafiti na Mtaalamu wa kimkakati Dkt.Hani Raslan

Harakati ya Nasser kwa Vijana yatoa maombolezo kwa Mtafiti na Mtaalamu wa kimkakati Dkt.Hani Raslan

 kwa huzuni na majonzi zaidi, kwa mioyo inayoamini hukumu ya Mwenyezi Mungu na kuridhika na kadiri yake, Harakati ya Nasser kwa Vijana inatoa Maombolezo ya kifo cha mtafiti na mtaalamu wa mikakati Dkt. Hani Raslan, mkurugenzi wa Kituo cha Al-Ahram kwa Mafunzo ya Kimkakati, Mtafiti imara kwa wasomi wa kisiasa na mfano wa kuigwa kwa waandishi wa habari, na rejeleo la watafiti katika masuala ya Kiafrika, na inatoa rambirambi zake za dhati kwa watu wote wa Afrika, na watu wa Misri pia Sudan haswa,  waliopoteza mtu mwenye maoni na hekima yenye busara, ni vigumu sana kumpata mtu kama yeye, mzalendo mwenye mwelekeo wa kitaifa, mwaminifu, aliyejitwika maswala ya bara la Afrika, na kuyashughulikia kwa utafiti, uchimbaji, uchambuzi kwa kina, na ufuatiliaji  kwa ujasiri, na kujivunia sana kwa historia yake, na alikuwa na vitabu vingi katika suala hilo, miongoni mwao ni kitabu “Sera za Julai.. Miaka Hamsini ya Mapinduzi” na kitabu “Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji.”

Mtafiti Mkuu "Raslan" aliishi akitetea suala bila pongezi au kukwepa hadi kifo chake, amani iwe juu ya roho yake safi, tukimwomba rehema na msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kumlipa kwa ukweli na uaminifu wake, usahihi wa kazi yake na juhudi zake kubwa katika maoni ya kimkakate na uchambuzi wa kisiasa. Mwenyezi Mungu amuingize peponi yake, na aipe familia yake subira na faraja.