Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ashinda Tuzo ya (5SDG)  kwa mwaka wa 2022 

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ashinda Tuzo ya (5SDG)  kwa mwaka wa 2022 

Bi. Ohinia Constance Enkoma, mhitimu wa kundi la tatu la Udhamini wa  Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa alipata  Tuzo Bora ya 5 SDG kwa mwaka wa 2022, na 5 SDG ni mpango wa tuzo za kimataifa kusherehekea mabingwa wa Dunia ambao wanabadilisha jamii na kuathari maisha na mazingira.

 Ohinia Constance alielezea ushindi wake wa tuzo hii ya kimataifa akisema: "Kweli, ikiwa unataka furaha, wasaidie wengine. Ninanyenyekea na nina furaha kubwa kuheshimiwa kwa kazi yangu; namshukuru sana Mwenyezi Mungu. Kushinda tuzo hiyo, ilikuwa shukrani kwa msukumo na usaidizi niliopokea kutoka kwa timu yangu katika Taasisi ya" Erudite "kwa ajili ya kuwawezesha  wanawake na familia, washauri, na majukwaa yanayolenga maendeleo kama vile Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa. Ninaahidi kwa maendeleo ili kuchangia kuifanya dunia  iwe mahali pazuri zaidi kwa wanawake na wasichana katika jamii ambazo hazijahudumiwa vizuri.” 

Imetajwa kuwa Ohinia Constance Ankoma ni mwalimu mtaalamu, mjasiriamali wa kijamii mwenye shauku ya kubadilisha maisha; Mwanamke mwenye maadili ya juu hujenga kituo cha maendeleo ya wasichana na wanawake vijana, Yeye pia ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Tassisi ya (Erudite) kwa ajili ya kuwawezesha wanawake,nalo ni shirika lisilo la faida na lililosajiliwa linalolenga wanawake nchini Ghana likiwa na lengo kuu la kuunda ulimwengu bora uliojaa fursa kwa wasichana na wanawake katika jamii zilizotengwa. Shirika lake linatoa uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake wa vijijini;na kuita ushirikishaji wa wasichana na wanawake vijana  katika kufanya maamuzi katika viwango vyote, inahimiza ufahamu wa afya ya kupata hedhi miongoni mwa wanafunzi wa kike katika jamii zisizojiweza ili kuwasaidia wasikose shule wakati wa hedhi kutokana na taarifa zao duni kuhusu mzunguko wa hedhi. 

Mnamo 2016, Ohinia alipata Diploma ya Elimu ya Msingi kutoka Chuo kikuu cha Agogo Al-Mashiakhia kwa Elimu ya Wanawake nchini Ghana.  Kisha alitaka kupata Shahada ya Kwanza katika Elimu ya Hisabati kutoka Chuo Kikuu cha Cape Coast, Ghana.  Pia ana cheti cha Uongozi wa Utumishi wa Umma na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Al-Mashiakhia , Ghana. 


Na kwa mchango wake wa ajabu katika maendeleo ya binadamu, aliteuliwa kuwa Balozi wa Nia Njema wa Kimataifa nchini Ghana mwaka wa 2018 na alitunukiwa kuwa mmoja wa Wanawake 60 Bora Barani Afrika katika Maendeleo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka 2022 na Wafadhili kwa Afrika.  Alichaguliwa pia kushiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu  mnamo 2022 huko Kairo, Misri. 

Ohinia  ana imani thabiti kwamba wanawake wana uwezo wa kuongoza upepo wa mabadiliko katika bara la Afrika, na anataka kuwa sehemu ya mabadiliko haya makubwa.  Ohinia anapanga kuanzisha vituo vya uwezeshaji  nchini Ghana na Afrika kwa ujumla ili kumwezesha kuendeleza wasichana na wanawake zaidi kupitia uingiliaji wa  kimkakati wa shirika lake. 

Katika muktadha unaoendelea na huo, Harakati ya Nasser kwa Vijana ilipongeza juhudi zinazofanywa na Ohenia na timu yake kusaidia kufikia malengo 17 ya maendeleo endelevu yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2015, haswa lengo la tano linalohusiana na usawa wa kijinsia: 'Kuhakikisha  usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana wote ifikapo 2030.