Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo na Ubalozi wa Ufaransa zamheshimu mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Bw. Ahmed Mukhtar, Mhitimu wa kundi la pili la Udhamini wa Uongozi wa Kimataifa wa Nasser na Mhitimu wa Mpango wa Urais wa kuandalia Watendaji Wanaohitimu kwa Uongozi kundi la Timu ya Al-Assar amezawadiwa, na hayo yametokea miongoni mwa shughuli za maadhimisho ya Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo na Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa kwenye makao makuu ya Ubalozi wa Ufaransa kwa ajili ya ushindi wa wahitimu wa kundi la Jenerali Mohamed Al-Assar kutoka Mpango wa uongozi wa kuandalia Watendaji wa kuongoza (EPLP), katika mtihani wa Diploma ya Lugha ya Kifaransa (DELF) na hiyo inakuja ndani ya mfumo wa ushirikiano wa pamoja kati ya Misri na Ufaransa Kupitia ushirikiano wa Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo "NTA" na Shule ya Usimamizi ya Ufaransa "L'ena ”, vilevile, Maadhimisho hayo yanakuja ili kuthibitisha juhudi za Chuo cha Taifa cha Mafunzo za kuwaandalia viongozi wenye uzoefu mbalimbali , wenye uwezo wa zana mbalimbali za mawasiliano na wanaoweza kushirikisha kwa ufanisi wa kuleta mabadiliko kwa nchi yao.
Ahmed Mokhtar anafanya kazi kama mkaguzi wa usalama wa anga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kairo.vilevile , ni kocha na mwamuzi wa midahalo katika baraza la kiutamaduni la Uingereza , katika kipindi cha Sauti ya Vijana waarabu na kisha programu ya Sauti ya Vijana ya eneo ya katikati .
Yeye pia ni mwanachama hodari na mwenye uzoefu kwenye jamii ya kiraia tangu kipindi cha Chuo Kikuu na hivyo kupitia Kamati ya makundi katika Umoja wa Wanafunzi, naye sasa ni mtafiti wa Shahada ya Uzamili ya Ujasiriamali ambapo alikuwa ameshahitimu kutoka Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Ain Shams mnamo 2005. licha ya kujifunza katika Taasisi ya kuwaandalia viongozi huko Helwan
Licha ya kupata kwake kozi ya Mkakati wa Usalama wa kitaifa, Kozi ya Usimamizi wa Migogoro, Majadiliano na kozi ya kutunga Maamuzi inayohusiana na kuelimisha masuala ya siasa kutoka Chuo cha Kijeshi cha Nasser, na baada ya kuhitimu kwake kutoka Chuo Kikuu, alifanya kazi katika taasisi za kimaendeleo kadhaa mpaka akawa mwanachama katika kamati ya Kiraia na Kazi ya kujitolewa kwenye Baraza la Kitaifa la Vijana mnamo 2010, naye Sasa ni mwanachama wa wakurugenzi wa chama cha Moameroon cha maendeleo ya jamii tangu 2016, pamoja na kufanya kazi katika uwanja wa kutoa mafunzo katika taasisi kadhaa.
Mokhtar alihitimu kutoka kwa kundi la pili la Mpango wa uongozi wa kuwaandalia Watendaji kwa Uongozi katika Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo, na kupitia kwake alipata kozi ya usimamizi wa migogoro kutoka Kituo cha GCSP cha Mafunzo ya Usalama na Siasa nchini Uswizi, na kozi za usimamizi na uongozi kutoka shule ya "L.ena " huko Ufaransa.
Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , katika toleo lake la pili, ulikuwa na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi na ulilenga viongozi vijana wa utendaji wenye taaluma mbalimbali na watendaji ndani ya jamii zao, wakiwakilisha mabara matatu, Afrika, Asia na Amerika ya Kusini, pamoja na kauli mbiu "Ushirikiano wa Kusini-Kusini".