Harakati ya Nasser kwa Vijana yampongeza Bi.Silga Marcola kushika nafasi ya Mkuu wa Jukwaa la Vijana wa Ulaya

Harakati ya Nasser kwa Vijana ilimpongeza Bi.Silga Marcola kushika nafasi yake mpya, ikimtakia mafanikio na ustawi zaidi.
Marccula alishinda baada ya kupita uchaguzi safi unaolenga kulinda demokrasia na kujitahidi kwa jukwaa la vijana la ushirikiano zaidi, Silga Marcola alishinda nafasi ya Mkuu wa Jukwaa la Vijana la Ulaya kwa mwaka wa 2021-2022.
Jukwaa la Vijana wa Ulaya ni jukwaa la mashirika ya vijana barani Ulaya, jukwaa huru na la kidemokrasia linaloongozwa na vijana linalowakilisha zaidi ya mashirika 100 ya vijana yakishirikisha mamilioni ya vijana kutoka kote ulimwenguni.
Silga alielezea furaha yake kwa nafasi hii, ana msisimuko ya kufanya kazi katika kutekeleza vipaumbele vya kimkakati, kulinda demokrasia, na kutafuta kongamano la vijana la ushirikiano zaidi.
Pia aliweka wazi kuwa yuko tayari sana kuanza na Baraza jipya la Idara lililojaa msisimko, hamasa na nguvu, na kutetea haki za vijana.
Mwishoni, alilishukuru Shirika la Skauti kwa kumfuatilia mnamo kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, na pia aliwashukuru wanachama wa Shirika hilo kwa kumchagua, akisema: "Nyinyi ni Nguzo, roho na uti wa mgongo wa Shirika" na kuwaahidi kuwa atafanya kazi kwa bidii na bila kuchoka kushirikisha kila mtu katika shughuli na kuwapa mahali pafaapo pa Usalama wa kufanya kazi na kupatia Ustawi.