Kampeni ya Vijana waarabu 75 ya kutambulisha Udhamini wa Nasser kwa Uongozi kwa maandalizi ya Toleo lake la la tatu

Kampeni ya Vijana waarabu 75 ya kutambulisha Udhamini wa Nasser kwa Uongozi kwa maandalizi ya Toleo lake la la tatu
Kampeni ya Vijana waarabu 75 ya kutambulisha Udhamini wa Nasser kwa Uongozi kwa maandalizi ya Toleo lake la la tatu
Kampeni ya Vijana waarabu 75 ya kutambulisha Udhamini wa Nasser kwa Uongozi kwa maandalizi ya Toleo lake la la tatu

Baadhi ya wahitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kundi la pili walizindua kampeni ya kuutambulisha,kwa ushiriki wa zaidi ya vijana wakiume na wakike 75 kutoka nchi mbalimbali za kiarabu kupitia  "ZOOM", na ushiriki wa wazungumzaji kutoka Misri, Tunisia, Chad na Sudan.

Msimamizi wa kikao na mjumbe wa timu ya vyombo vya habari vya kimataifa katika Udhamini wa Nasser 

" Al_ Zubair Al Barki" kutoka Libya alifungua mazungumzo kwa kukaribisha mahudhurio na kutoa utangulizi kuhusu lengo la Udhamini na kuwatambulisha wazungumzaji,

alianza hotuba yake kwa kutambulisha Udhamini na historia yake na akasema kwamba: Udhamini wa Nasser ni mmojawapo wa Udhamini muhimu zaidi ulioandaliwa kwa Misri na Wizara ya Vijana na Michezo pamoja na Ufadhili wa  Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El Sisi.

 Na kutoka Misri, Mahamoud Labib alisema: Udhamini wa Nasser ni kiongozi wa kweli mwenye uwezo wa mabadiliko katika nchi na jamii yake kwa kuchanganya na wafanya uamuzi huko Misri katika nyanja mbalimbali,  kuzungumza nao kuonyesha uzoefu wao wa kipekee uliochangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha Uongozi kwa washiriki, na haukuwa na vikao vya kutambulisha vya kitaaluma tu.

Sukain Babiker kutoka Sudan alimshukuru Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri Dkt, Ashraf Sobhy anayehimiza Udhamini na alikuwepo kila wakati na yupo karibu na washiriki, pia alizungumzia uzoefu wake wa kipekee katika Udhamini na jinsi malengo yake yalihakikishwa kutoka ushiriki na alitoa baadhi ya mashauri kwa waombaji wapya.

Na Udhamini katika toleo lake la tatu unalenga kuangazia jukumu la vijana wasiofungamana upande wowote katika kuendeleza ushirikiano wa Kusini_ Kusini wakati Ulimwengu unaobadilika kwa haraka na jinsi ya kuendeleza ushirikiano huo kupitia vijana kama mtaratibu mzuri na endelevu pamoja na kuzingatia jukumu la mwanamke; kwa hiyo kauli mbiu ya Udhamini ya mwaka huu ni  Ushirikiano wa Kusini-Kusini na Vijana wasiofungamana upande wowote. 

Imepangwa kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa utaanza mnamo Mei 28 ujao, na utaendelea kwa muda wa siku 15.