Harakati ya Vijana wa Nasser nchini Tunisia inaandaa kikao cha kawaida kinachoitwa "Hadithi za mafanikio ya vijana wa Kiafrika ulimwenguni"
Imetafsiriwa na: Marwa Mansour
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Ndani ya muktadha wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana ya Kimataifa, Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Tunisia na Ofisi ya Tunisia, Shirika la Vijana la Jusoor, kwa kushirikiana na Jukwaa la Vijana wa Kiarabu kwa Maendeleo Endelevu na Chama cha Vijana cha Sidi Hussein, wanaandaa kikao cha kawaida kinachoitwa hadithi za mafanikio ya vijana wa Kiafrika ulimwenguni. Leo, Alhamisi, Agosti 12, 2021 saa kumi jioni saa za Kairo, kupitia jukwaa la Zoom.
Ili kuhudhuria kikao, Mnaweza kufikia kupitia kiungo kifuatacho:
https://us02web.zoom.us/j/81844940287...
Kikao hicho kitawasilisha uzoefu wa mifano kadhaa ya vijana wa kiraia na wa Kiafrika na viongozi katika ngazi ya kimataifa ili kuthamini kazi ya wanaharakati na kuchochea ushiriki wa vijana katika kazi ya kujitolea.