Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ashinda jina la mtangazaji bora zaidi wa Sudan kwa 2021

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ashinda jina la mtangazaji bora zaidi wa Sudan kwa 2021

Miezi michache iliyopita, Mtangazaji wa Sudan "Lina Zine El Abidine " alishinda Udhamini wa Oakridge kwa utangazaji wa televisheni huko Dubai kwa mwaka wa 2021, na wakati huo tulimwuliza kuhusu ndoto yake, akisema : "Natamani kuwa mtangazaji mwenye ushawishi katika taifa la kiarabu na Duniani kote , na kuwa miongoni mwa watangazaji hodari, wa pekee, na bora zaidi , na kutangaza kupitia maudhui ya vyombo vya habari kila kinachohudumia nchi na raia wangu".

Na leo anasonga kwa mwenendo wa kujiamini kuelekea kuhakikisha ndoto, Na anapata jina la mtangazaji bora wa Redio katika kura ya maoni ya jukwaa la Wakeb la kidijitali la Sudan kwa mwaka wa 2021 miongoni mwa wapiga kura zaidi wanaofika 29% miongoni mwa kundi la watangazaji mashuhuri wa Sudan kama:  Lamiaa Mutawakil aliyepata kura 26%, Nadine Aladdin aliyepata kura 25% na Fatma Kabashi alipata kura 20% .

Alabdin ni mmoja wa wanaharakati mashuhuri wa mitandao ya kijamii, na anafanya kazi kama mtangazaji wa vipindi vya redio na televisheni. Alianza safari yake ya vyombo vya habari kama mtangazaji wa redio tangu 2012 kwa programu ya " Alaa El tarik" kwa muda wa miaka saba, kisha programu ya " Basat Al_ Reeh " ambapo alishinda tuzo ya programu bora zaidi ya Utalii ya redio katika taifa ya kiarabu, na alizawadiwa kwa kituo cha vyombo vya habari cha Utalii cha kiarabu katika Ufalme wa Oman, Na alihamia televisheni katika programu ya " Sabah Al _ Shorouk " mnamo 2019 na alikaa huko zaidi ya mwaka mmoja na miezi saba, kisha akahamia kufanya kazi kwa kituo cha redio kinachoitwa pro.Fm 106, 6 kama mtangazaji kwenye programu ya uandishi wa habari ya aina mbalimbali.

Alabdin pia alifanya kazi mnamo mwaka uliopita katika uwanja wa uchunguzi wa uandishi wa habari, Alitangaza takriban vipindi nane vilivyoonyedhwa katika mwezi wa Ramadhani 2021 kupitia programu ya " Nogom Fi Alfakh" na ilifika kiwango cha utazamaji cha juu zaidi huko Sudan. 

Ni vyema kuashiria kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la pili ulizindua mjini Kairo, Juni 2021 pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El _sisi na kwa kauli mbiu ya " Ushirikiano wa Kusini -Kusini" na uliwalenga viongozi wa  vijana wa kutekeleza wenye taaluma mbalimbali na ushawishi mkubwa katika jamii zao kama wawakilishi wa taifa zao kutoka mabara matatu: Asia, Afrika na Amerika ya Kusini; kuimarisha mwenendo wa Umoja wa Afrika; ili kuwekeza katika vijana na kuhakikisha malengo ya maendeleo ya Umoja wa mataifa na ushirikiano wa kusini Kusini.

Mwishowe, mshikamano wetu wote kwa raia wa Sudan na vijana walioahidiwa, wasomi, waaminifu na wenye upendo kwa taifa wao, tunaendelea kuwa na matumaini kuwa  Mwenyezi Mungu ahifadhi familia, ardhi na mtoto, na Utulivu, Usalama, Amani na Ustawi zirudishe nchini Sudan kwa michango ya vijana wake waaminifu.