Mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Tunisia akutana na Rais wa Burundi

Bi.Kholoud Bin Mansour, mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Tunisia, alikutana na Mheshimiwa Bw. Evariste Ndayishama, Rais wa Burundi wakati wa matukio ya mkutano Na.1080 wa Baraza la Amani na Usalama la Afrika, ambayo Burundi inachukua urais wake mnamo mwezi huu wa Aprili.
Mkutano ulifanyika katika nyumba ya Mheshimiwa Rais huko mji mkuu wa zamani wa Burundi, Bujumbura, ndani ya ujumbe wake kama Balozi wa Amani wa Umoja wa Afrika. Na pia, ziara hiyo ilijumuisha kufanya mikutano na watu rasmi nchini Burundi.