Udhamini wa Nasser washinda tuzo ya hamasa ya Nchi ya 2021
Mwandishi wa habari wa gazeti la Al_ Gomhuria, Mtafiti wa chuo katika uwanja wa elimu ya Folklor na Anthropolojia ya kiutamaduni katika kitivo cha mafunzo ya juu ya Afrika katika Chuo Kikuu cha Kairo alishinda tuzo ya hamasa ya nchi kuhusu kitabu chake kiitwacho " vipengele maarufu vya muziki vinavyohusiana na mazingira ya Nuba ... Al _Tanbura kama mfano" ambapo alijadili usomi wa utafiti wa moja ya ala za muziki ya nyuzi za kiutamaduni za Nuba za Misri , inayojulikana nchini Misri kwa Tanbura na huko Nuba kwa "Kasar"
Abu Shanab katika usomi huo uliojumuisha kazi za marejeleo na uwanjani alijadili ala hiyo kwa mujibu wa ( dhana ya ala, maelezo ya ala, njia ya sauti, udhibiti wa ala, njia ya kucheza, mahali pa kuwepo kwa ala, na mipaka ya ueneaji wake, ukubwa wa ala, misamiati ya ala, sifa za ala , wachezaji wa ala, na muktadha wa kiutamaduni ambapo ala hiyo inatumika, nafasi ya ala katika vikundi maarufu wanayoitumia, majina ya ala,vipengele vya ala,aina za ala, malighafi ya kamba, ala ya kuchezea, uainishaji wa ala, historia ya ala, funguo za ala, ukubwa wa masanduku ya ala na vipengele vingine vya maelezo pamoja na kueleza uhusiano na tofauti baina ya ala ya Tanbura na Al_ Semsemea inayoenea katika miji ya mfereji.
Abu Shanab anasimulia safari yake na urithi wa kiutamaduni ambao akawa anapenda kwa kiasi kikubwa; kwani alielezea kupitia hiyo vipengele vingi vya kiutamaduni ambavyo vinamulezea kiwango cha uhusiano wa binadamu na urithi wa kiutamaduni unaotolewa naye na kupokea katika wakati huu huu, akisema: kwamba kupitia kazi yangu katika uwanja wa uandishi wa habari katika baadhi ya maeneo ya mipaka haswa ya Kusini kama Nuba, Halayeb na Shalateen, nilikuwa nikikusanya na kufuatilia maudhui mbalimbali ya kiutamaduni ya Misri yanayohusu kila eneo; Na hiyo kutokana na kukaa kwangu huko kwa kipindi ambacho kinaweza kuchukua kati ya wiki moja na siku kumi kwa kila ziara niliyoifanya ; kwa mujibu wa kuniwajibiwa kwa uandishi wa habari, na baada ya kuchapisha makala nyingi za kiutamaduni katika suala hilo, nilitaka kujua zaidi katika uwanja huo wa kitaalamu katika masomo ya watu, na kwa kweli nilijiunga Chuo cha Sanaa, na nilisoma asili ya elimu hiyo na matawi yake tofauti kwa makini, na mnamo wakati huo nilitolewa uzalishaji wangu wa kwanza wa fikra kwa kauli mbiu " Desturi za Hanaa ya wanaume katika mji wa Nuba nchini Misri" na baada ya kupata shahada ya Diploma katika Chuo cha Sanaa katika kitengo cha mitaala Folklor na mbinu za kuhifadhi kitabu changu kingine kilitolewa ambacho kilikuwa mradi wa Diploma na hamasa ya moja kwa moja ya baadhi ya Maprofesa waliobobea kinachoitwa " vipengele maarufu vinavyohusiana na tabia za mzunguko wa maisha ya wanubi wa Misri: Utafiti wa mji wa thabiti katika baadhi ya maeneo ya Kairo na Aswan.
Baada ya ushiriki wangu katika utafiti wa kisayansi kwa anwani ya " Ala za muziki za Misri ni chanzo cha utafiti wa binadamu ...Tanbura ya Afrika kama mfano na hiyo katika mkutano wa kwanza wa kisayansi wa kimataifa katika Chuo cha Sanaa, nilikamilisha utafiti huo hadi kikawa kitabu ambacho nilishinda kupitia kwake tuzo la hamasa la Nchi , Na kwa wakati na kuongeza upendo wangu wa urithi wa kiutamaduni wa Nuba, Nilifikiri katika wazo lingine ambayo matokeo yake yalikuwa kupata vitabu viwili, ambavyo nilijadili utafiti wa Anthropolojia wa mmoja wa wataalamu wa kigeni waliotembelea eneo la Nuba mwanzoni mwa karne ya 19 kwa anwani ya " Mkusanyiko wa vipengele vya urithi wa watu kutoka vitabu vya wanasafiri na wataalamu katika Nuba nchini Misri...Burkchardt kama mfano" sehemu ya kwanza na ya pili.
Mtafiti Mohamed Abo Shanab aliashiria kuwa ushindi wake wa tuzo hizo muhimu za kisayansi zinazotolewa daima kutoka nchi kwa watafiti mbalimbali mashuhuri katika nyanja mbalimbali na elimu za kibinadamu ni kama medali ya heshima ambayo mtu atajivunia katika maisha yake yote , na kwa upande mwingine Heshima hiyo inaakisi kiwango cha ujali wa taasisi za kisayansi na kiutamaduni kwa mfumo wa utafiti wa kisayansi kwa jumla na kazi endelevu ya kuendeleza nchini Misri; kwa lengo la kuhudumia jamii na kuhakikisha maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali.
Inatajwa kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la pili ulizingatia usawa wa kijinsia katika mchakato wa uteuzi, uliwalenga vijana 100 kwa asilimia 50 hadi asilimia 50 ya jinsia zote mbili kutoka viongozi wa vijana wenye ushawishi katika jamii zao kama wanaharakati wa jamii, viongozi watendaji ambao wana taaluma mbalimbali, washiriki wa kitivo katika vyuo vikuu, watafiti katika vituo vya kimkakati, wafanya uamuzi , pamoja na kuzingatia maeneo ya mipaka; ambapo ulitegemea mifumo kadhaa na vigezo katika mchakato wa kuteua washiriki , ulizingatia kwa uwazi na umakini tofauti za kijiografia , kiwango cha elimu, kitaasisi, athari za kijamii, kazi, na hata Kiutamaduni, ambao waombaji waliweza kuonyesha ;kushiriki katika Udhamini huo.