Programu ya Julai ya Mawazo ya Kwanza .. Kama Maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 5 ya kuanzishwa kwa Harakati ya Nasser kwa Vijana

Programu ya Julai ya Mawazo ya Kwanza .. Kama Maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 5 ya kuanzishwa kwa Harakati ya Nasser kwa Vijana

Sambamba na sherehe za watu huru za maadhimisho ya miaka 71 ya Mapinduzi matukufu ya Julai, na sherehe za Misri za kuadhimisha miaka 67 ya kutaifishwa kwa Mfereji wa Suez, Harakati ya Nasser kwa Vijana, kwa ushirikiano na Taasisi ya Afrika ya Maendeleo na Kujenga Uwezo, iliandaliwa  "Programu ya Julai ya Mawazo ya Kwanza," kuanzia Julai 23 hadi Julai 26, wakati ambapo hiyo inalingana na maadhimisho ya miaka 5 kwa kuanzishwa kwake.

Hiyo ilikuja ndani ya mfumo wa Mpango wa Mshikamano na Amani wa Taasisi ya Afrika kwa Maendeleo na Kujenga Uwezo, ambapo Taasisi hiyo inalenga kufufua na kuimarisha utamaduni wa mshikamano na roho ya ushiriki kati ya watu, kwa kuzingatia dhana ya Ushirikiano wa Kusini-Kusini, tena kwa kuzingatia kanuni zilizowekwa na hayati kiongozi Gamal Abdel Nasser katika Global South kwa ujumla, na haswa Barani Afrika akiwa “Baba wa Afrika na mkombozi wake” na mwanzilishi wa Umoja wa Afrika na kaka yake Nkrumah, ambayo iliyosababisha kuwepo kwa " Jumuiya ya Nchi Huru za Afrika 1963".

Na programu iliendelea kwa muda wa siku nne, safari ilianza kwa ziara kwenye kaburi la kiongozi Gamal Abdel Nasser na kutoka hapo kwenda kikao Cha ufunguzi katika makumbusho yake ,
kisha Taasisi ya Kiafrika kwa maendeleo na ujenzi wa uwezo ilikuwa mwenyeji wa matukio mengine ya programu , ikihudhuriwa na kikundi cha wasemaji na wanafikra , miongoni mwao: Mhandisi Abdel Hakim Gamal Abdel Nasser , mwana wa marehemu kiongozi Gamal Abdel Nasser , Prof. Gamal Sheiha Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Taasisi ya Kiafrika , na Mwenyekiti wa kamati ya elimu na utafiti wa kitaifa , Dkt. Hassan Mousa , Atta Hanna Askofu Mkuu wa Kanisa la Orthodox huko Jerusalem , Profesa. Gamal Shuqra , Profesa wa Historia Ua Kisasa katika Chuo Kikuu Cha Ain shams , Dkt. Mohamed Talba Mwenyekiti wa Taasisi Mwelekeo kwa Ushauri na Utafiti , Dkt . Mohamed El- Saeed Idris Mashuri wa kitaaluma katika kituo Cha Ahram Cha Masomo ya siasa na mikakati , Prof. Gouda Abdel Khaleq , Profesa wa Uchumi katika Chuo Kikuu Cha Kairo na Waziri wa Usharikiano na Sheria za Jamii wa zamani , Prof. Hassan Heikel Mtalamu wa Uchumi na Mwanachama wa Ofisi kuu ya Chama cha Nasser , Prof. Gamal Abu Aita , Waziri wa Kazi na Uhamiaji wa zamani , Dkt. Nadia Gamal El-Din Profesa wa Misingi ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Juu cha Elimu na mwandishi wa habari Youssef Al - Qaeed , tena Profesa Seham Negm , Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake na Jamii .

Kikao cha kwanza kilihusu "Mapinduzi ya Julai Hadithi na Kumbukumbu", kisha shughuli za siku ya pili zilishughulikia kikao kilichoitwa "A Future Reading kwa Mapinduzi ya Julai", kilihusu hati za kiakili za Mapinduzi ya Julai na kanuni za Mapinduzi ya Julai, tena kanuni za Maafisa Huru, kikiwemo kitabu cha Falsafa ya Mapinduzi na Mkataba, pamoja na kushughulikia sifa za maisha bora ya kidemokrasia ya serikali ya Mapinduzi ya Julai. 

Katika shughuli za siku ya tatu, vikao vilishughulikia Mapinduzi ya Julai na nafasi ya uchumi katika uboreshaji wa kijamii, ambapo majadiliano yalihusu mtazamo wa maendeleo wa Mapinduzi ya Julai, dira ya Mapinduzi ya Julai na nafasi yake katika Mapinduzi hayo kwa Uboreshaji wa kijamii wa tabaka la wafanyikazi kati ya zamani na zijazo, wakati shughuli za siku ya nne zilikuwa tajiri sana kwani zilishughulikia shoka kadhaa muhimu,  miongoni mwao ni elimu kama nyenzo mojawapo ya maendeleo ya kijamii, na faida zilizopo kwa wanawake kutoka kwa Mapinduzi ya Julai,na vikao hivyo vilihitimishwa kwa kikao cha Kutaifisha Mfereji wa Suez kama mfano muhimu wa kuweka mabadiliko.