Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ashiriki kwenye Tamasha la Kimataifa la Monodrama huko Carthage

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ashiriki kwenye Tamasha la Kimataifa la Monodrama huko Carthage

Imetafsiriwa na: Shahd Ahmed Shawky
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr 

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, toleo la pili (2021), Yassine Fathali, alishiriki katika Tamasha la Kimataifa la Monodrama huko Carthage katika kikao chake cha nne, kilichofanyika kutoka 13 hadi 16 Mei 2022, nchini Tunisia.

Tamasha hilo linalenga kuongeza hamasa katika sanaa ngumu ya uigizaji inayotegemea utendaji wa muigizaji mmoja, na tamasha hilo liliweza kuvutia zaidi ya onesho moja la kisanii kutoka nchi mbalimbali duniani.

 Usimamizi wa tamasha ulikuwa umempa Fattahli jukumu la kusimamia timu ya kujitolea ya shirika, kwa kushirikiana na Shirika la Skauti la Tunisia, na Shirika la Vijana la Jusoor. 

 Ni muhimu kutambua kwamba "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" unalenga kujenga kizazi kipya cha viongozi wa mabadiliko ya vijana na maono kulingana na mwelekeo wa urais wa Misri katika nchi mbalimbali kupitia ushirikiano, pamoja na kuunganisha viongozi wa vijana wenye ushawishi mkubwa duniani na mafunzo, ujuzi muhimu na maono ya kimkakati.