Mhitimu wa Udhamini wa Nasser ni Mzungumzaji katika Kongamano la Amani ya Dunia la Umoja wa Mataifa

Mhitimu wa  Udhamini wa Nasser ni Mzungumzaji katika Kongamano la Amani ya Dunia la Umoja wa Mataifa

"Mateo Villamil" Mhitimu wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni Mzungumzaji katika Kongamano la Amani ya Dunia la Umoja wa Mataifa

Hotuba yake ilianza kwa kuwashukuru kundi la Kongamano ya Amani la Dunia, na aliwataja haswa marafiki zake wawili, Daniela na Kubla, kisha hotuba yake ilikuwa pamoja na "Uaminifu wa Kiakili: Jiwe la Msingi la Amani ya Dunia". ambapo anasema:

 ‏

"Ndugu Waheshimiwa, kama mjuavyo, Amani inahitaji uadilifu wa kijamii, na uadilifu wa kijamii unahitaji Maendeleo Endelevu, na ningependa kushiriki nyote maoni yangu yote kuhusu suala hilo muhimu, naona kuwa ubinadamu unahitaji kuharakisha na kuchapisha mafunzo ya kitaaluma kuhusu suala la Endelevu.

Pia, tunapaswa kuungana na kuhakikisha utu na riziki za maisha kwa wote kama kitendo kimoja cha uadilifu, na ni lazima tubadilishane makundi tofauti ambayo ni makubwa zaidi ya maarifa ya kimbinu yenye faida kubwa kutoka Duniani kote, na haina shaka kuwa ubadilishanaji huo ni jambo muhimu sio tu kwa Ulaya, bali pia kwa pembezoni mwa mpangilio wa Dunia ambapo tunaupata.

Vilevile, ninapendekeza sana kuzingatia mifumo ya taarifa za kiuchumi, kama vile mfumo wa Stafford Bear katika enzi ya Chile enzi ya Allende, au mfumo wa nchi ya China yenyewe, au mfumo wa Amazon mnamo wa wakati huu wa kisasa.

Hatimaye, ni muhimu kutambua kuwa vijana wana jukumu katika kujadili kwa ukosoaji na kuboresha kiasi hicho cha hekima ya kibinadamu, licha ya wajibu wa kutekeleza mawazo yao kwa vitendo kwa Uaminifu, Udhibiti na Amani".

Sote tunajivunia hotuba ya mwenzetu mpendwa Matteo, ambapo alionesha sauti zetu, na ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa iliyozinduliwa mnamo Juni 2021, ulikuwa ukilenga viongozi watendaji wenye taaluma tofauti katika mabara matatu ya Asia, Afrika na Amerika Kusini, pamoja na Ufadhili wa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.