Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ashiriki katika warsha ya mafunzo kuhusu maandalizi ya malalamiko kwa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu
Imetafsiriwa na: Rawda Sallam
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Yassin Fathali, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kundi la pili, alishiriki katika warsha ya mafunzo kuhusu kuandaa malalamiko kwa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, ndani ya mpango wa "Viongozi Mpya katika uwanja wa Haki za Binadamu", ulioandaliwa na Taasisi ya Kiarabu ya Haki za Binadamu kwa kushirikiana na Open Society Foundation, chini ya usimamizi wa: Dkt. Hafiza Choucair, Profesa wa Sheria ya Umma na Rais wa Kamati ya Sayansi ya Taasisi ya Kiarabu ya Haki za Binadamu, Dkt. Wahid Ferchichi, Profesa wa Sheria ya Umma, na Bw. Imad Zouari, mtaalamu wa utetezi, mnamo tarehe Jumatano, Juni 22, 2022, katika Hoteli ya Afrika huko Tunis.
Mafunzo ya kiufundi kuhusu utetezi na mifumo ya kushawishi pia ilitolewa kando ya semina.
Ni vyema kutajwa kuwa "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" inalenga kujenga kizazi kipya cha viongozi wa mabadiliko ya vijana na maono kulingana na mwelekeo wa urais wa Misri katika nchi mbalimbali kupitia ushirikiano, pamoja na kuunganisha viongozi wa vijana wenye ushawishi mkubwa duniani na mafunzo, ujuzi muhimu na maono ya kimkakati.