Ufunguzi wa Hifadhi ya Kwanza ya Mlima Duniani kwa Makazi ya Mnyama Bongo

Imetafsiriwa na: Marwa Yasser Mahmoud
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Jana, Waziri wa Utalii na Wanyamapori Najib Balala, kwa kushirikiana na Huduma ya Wanyamapori ya Kenya, Huduma ya Misitu ya Kenya, na Hifadhi ya Wanyamapori ya Mlima Kenya, walizindua hifadhi kubwa zaidi ya mlima ulimwenguni na eneo la ekari 776, limelotengwa kwa ajili ya mmoja wa wanyama adimu zaidi wa paa duniani, ambaye hupatikana tu nchini Kenya.
Bongo ni miongoni mwa wanyama wa kipekee nchini Kenya, ambapo wanyama 100 pekee ndio waliosalia porini, na anatajwa kuwa mnyama aliye hatarini kutoweka ambaye ni mzaliwa wa misitu ya kitropiki ya Kenya (Mlima Kenya Forest, Iburo, Mau na Aberdares).
Najib aliongeza: "Aina hii ya paa wakubwa ilikuwa ikizunguka kwa idadi kubwa hapo awali, lakini ilikumbwa na kupungua kwa kasi kwa idadi yake tangu miaka ya 1950 kutokana na uwindaji haramu, biashara ya wanyama hai, uwindaji wa wanyama walao nyama, na magonjwa, hasa mlipuko wa ugonjwa wa tauni ya ng'ombe katika miaka ya 1980."
Hata hivyo, hadi sasa hawajapokea kiwango sawa cha tahadhari ya kimataifa kama safari za "Tano Kubwa", ambazo kwa sehemu zimechangia kupona kwa idadi yao.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za wanyama pori nchini Kenya, chini ya wanyama 100 wa bongo wanasalia porini.
Kulingana na makadirio ya Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN), takwimu hii inaweza kuendelea kupungua isipokuwa hatua za makusudi zitachukuliwa kushughulikia vitisho.