Marekani na Umoja wa Afrika zasaini mkataba wa maelewano

Marekani na Umoja wa Afrika zasaini mkataba wa maelewano

Imetafsiriwa na: Malak Abd-Elnasser
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mohamed, walithibitisha ahadi yao ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano katika afya ya umma kwa kusaini mkataba wa maelewano kuhusu ushirikiano wa nchi mbili wakati wa Mazungumzo ya ngazi ya juu ya Marekani na Marekani huko Washington.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilieleza kuwa Sherehe hiyo iliangazia ushirikiano mkubwa kati ya serikali ya Marekani na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti Magonjwa (ACDC) na kuruhusu mahusiano ya baadaye kuhuishwa.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa mkataba huu wa ushirikiano unaboresha ubia unaosaidia na kuweka misingi ya taasisi za kitaifa za afya ya umma, unaendeleza utafiti kwenye uwanja wa afya ya umma barani Afrika, unaendeleza makada wa afya, kuimarisha kujitolea kwa sekta binafsi, na unaruhusu kujenga uwezo katika uwanja wa sekta ya chanjo na mahitaji mengine ya usalama wa afya. 

Chanzo hicho hicho kimebainisha kuwa maeneo haya yote ni muhimu katika kukabiliana na mlipuko wa janga la Covid-19, na kueleza kuwa "wanaunga mkono wito wa Umoja wa Afrika wa mfumo mpya wa afya ya umma barani Afrika, na usalama wa afya duniani, baada ya janga la COVID-19."

Kituo cha Afrika cha Kudhibiti Magonjwa (ACDC) kinachukua jukumu la kuongoza katika ngazi za bara na kimataifa katika kupambana na janga hili.

Ushirikiano kati ya Marekani na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti Magonjwa umebadilika kwa kiasi kikubwa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho mnamo mwaka 2015, taarifa hiyo ilisema, ikisisitiza kuwa kuimarisha mahusiano hayo muhimu kunaonesha lengo lao la pamoja la kuimarisha mifumo ya afya barani Afrika.

Kwa upande mwingine, Belkin na Mohamed walifanya majadiliano yaliyolenga umuhimu wa ushirikiano thabiti kati ya Marekani na Tume ya Umoja wa Afrika kushughulikia changamoto za kawaida kama vile janga la COVID-19, usalama wa afya, mabadiliko ya hali ya hewa, na haja ya mabadiliko ya nishati ya haki.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili pia yalizungumzia haja ya kuendeleza ukuaji wa uchumi wa dunia na demokrasia imara, kwa mujibu wa taarifa hiyo, akiongeza kuwa Blinken alisisitiza msaada wa Marekani kwa juhudi za Umoja wa Afrika za kukuza amani na utawala bora barani Afrika.