Uzinduzi wa muungano wa vyuo vikuu vya Afrika kwa kuzingatia ujasiriamali

Imetafsiriwa na: Tarek Said
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (UNECA) na washirika wake walizindua Umoja wa Vyuo Vikuu vinavyovutiwa na Ujasiriamali barani Afrika wakati wa Mkutano wa Mkoa wa Afrika juu ya Maendeleo Endelevu.
Dkt. Cheikh Mahamadou Mbaki Lo, profesa wa afya ya umma katika Chuo Kikuu cha Anta Diop cha Dakar nchini Senegal, alisema muungano huo utaruhusu vyuo vikuu vya Kusini, na rasilimali chache, kuanzisha ushirikiano wa vyuo vikuu ili kubadilishana na kuziba mapengo.
Mbaki Lo, ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Utafiti wa Sayansi la Senegal, alisema Muungano wa Vyuo Vikuu vinavyovutiwa na Ujasiriamali barani Afrika una lengo la kuwezesha kubadilishana data, uzoefu na mazoea mazuri kati ya taasisi za vyuo vikuu na taasisi za utafiti barani.
Alisema kuwa chombo hiki kitawezesha kwa dhati motisha ya vyuo vikuu na kuimarisha ushirikiano na makampuni.
Msomi huyo wa Senegal alisema kuwa muungano huo utawezesha kuanzishwa kwa ushirikiano wa kikanda kati ya vyuo vikuu na makampuni kupitia chombo rahisi ambacho kitawezesha mwingiliano na maamuzi.
Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (UNECA) na washirika wake waliandaa Mkutano wa 8 wa Afrika kuhusu Maendeleo Endelevu kutoka 3 hadi 5 Machi huko Kigali chini ya kauli mbiu "Kujenga Baadaye Bora: Afrika ya Kijani, Umoja, Utulivu tayari kufikia Ajenda ya 2030 na Ajenda 2063".
Mkutano huu wa Afrika ni mojawapo ya njia tatu zilizopewa mamlaka na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kufuatilia, kutathmini na kuchochea shughuli zinazolenga kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu yaliyojumuishwa katika Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu iliyopitishwa na Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2015.
Mkutano huo wa siku tatu unalenga kuwezesha kujifunza, ikiwa ni pamoja na kubadilishana mbinu, uzoefu na masomo yaliyojifunza kutokana na tathmini ya hiari ya kitaifa, tathmini ya hiari ya ndani na juhudi za utekelezaji.