Misri Yataka Kuishi Kwa Amani Pamoja na Wote

Imetafsiriwa na/ Enas Abd El-Basset
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Swali la mzungumzaji : Siku hizi watu wanajiuliza – na wana haki ya kujiuliza – ni nini lengo la kisiasa la ziara yako ijayo huko nchini Urusi? Je, ziara hii itakuwa hatua ya kuimarisha mahusiano kati ya Nchi za Kiarabu na serikali ya Sovieti? Je, ziara hii inawezekana kuwa na lengo fulani katika sera ya Marekani kuelekea Mashariki ya Kati? Je, ziara hii inapingana na mapambano ya nchi ya Kiarabu dhidi ya kanuni za Kikomunisti?
Rais Nasser: hakuna lengo la kisiasa kwa vitendo, lakini lengo lake kuu ni kwamba Misri inaongoza sera na tabia zake kutoka kwake mwenyewe mbali na ushawishi wowote au shinikizo la nje, na kwamba Misri inaweza kuamua kile inachotakia inapotakia, na kwamba haijaunganishwa na sera inayotangazwa na nchi kubwa.
Lengo la ziara hiyo kuwa Misri inataka kuishi kwa Amani pamoja na wote, na kuona Amani ikieneza ulimwenguni kote.
Kuhusu suala la karibu kati ya Nchi za Kiarabu na serikali ya Sovieti, bila shaka kwa nchi za Kiarabu ni suala linalotegemea sera ya kila nchi ya Kiarabu, lakini nadhani ziara hii itatufungulia nafasi kubwa katika uwanja wa kiuchumi, Kwa mfano: mkutano wa Bandung na mkutano wangu wa kibinafsi na “Cheyenne Lay” ulituwezesha kuondoa mazao yetu ya ziada ya pamba, kwa hivyo China imenunua pauni milioni 12 za pamba yetu ya ziada ambayo hatukuweza kuuza msimu huu.
Na ukiniuliza kama ziara hii inaweza kuwa na lengo katika sera ya Marekani kuelekea Mashariki ya Kati, basi naomba nikiulize, sera gani ya Marekani inaelekea Mashariki ya Kati? Kwa mfano: Sera yake ni nini kuhusu Lebanon na Syria?
Mimi niko hapa Misri, nafikiria masilahi ya Misri kwanza na zaidi ya yote… Hili ni jukumu langu la kwanza, na bila shaka napendelea Misri kuliko Marekani, na Misri kuliko Urusi, jambo la muhimu ni kwamba kila kitu ninachofikiria ni faida ya nchi yangu.
Misaada ya Marekani ambayo baadhi ya watu wanadhani kuwa inaweza kuathiri sera zetu, ni kujua kwamba Mapato yetu ya Kitaifa ni takribani pauni milioni 890, bajeti yetu mwaka huu ni imefikia pauni milioni 238, na misaada ya Marekani – ambayo ni kwa ajili ya huduma – ni pauni milioni 13 tu, misaada ambayo Marekani inatoa kwa Israeli, basi misaada hiyo ni nini mbele ya mamilioni ambayo tuliweka kwa ajili ya miradi mbalimbali? Baadhi ya mifano ni hii:
Mradi wa Umeme wa Aswan ulitugharimu pauni milioni 40.
Kujenga Shule Mpya, kwa kiasi pauni milioni 40.
Mradi wa Mbolea , kwa kiasi pauni milioni 25.
Mradi wa Chuma, kwa kiasi pauni milioni 17.
Mradi wa Barabara, kwa kiasi pauni milioni 12.
Mageuzi ya Ardhi ya Porini, kwa kiasi pauni milioni 12.
Maji ya Kunywa kwa Vijiji, kwa kiasi pauni milioni 12.
Jumla ya Vitengo, kwa kiasi pauni milioni 8.
Idara ya Uhariri, Pauni milioni 8.
Na kuhusu swali lako kama ziara hii inapingana na mapambano ya Nchi za Kiarabu dhidi ya kanuni za kikomunisti au la, nasema: Sisi hapa Misri tunapigana dhidi ya ukomunisti, hii ni jambo moja na ziara ni jambo lingine; Ukomunisti nchini Misri ni kuvunja sheria. Na Balozi Mrusi katika suala hili aliniambia kuwa hawana mahusiano yeyote na Wakomunisti waliopo Misri, na kwamba wanaona Ukomunisti ni madai tu. Na ingawa Misri tunawakamata wakomunisti na kuwapeleka mahakamani, hii haijazuia CIA, haikutuzuia kupelekea kutembelea Urusi, na ninaiona kama mojawapo ya hatua ambazo Urusi inachukua sasa ili kuimarisha mahusiano yake na nchi zote za ulimwengu.
Sehemu ya mzungumzo ya Rais na “Ahmed Shuman”.
Mhariri wa Gazeti la Lebanon la Al-Garida , mnamo Agosti 16, 1955.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy