Kumbukumbu ya kupita miaka 55 kwa uhuru wa Jamhuri ya Mauritius

Kumbukumbu ya kupita miaka 55 kwa uhuru wa Jamhuri ya Mauritius
Mauritius ilibakia makazi ya Uholanzi kutoka 1598 hadi 1710, kisha ikawa koloni la kiufaransa mnamo 1715 baada ya Uholanzi kuachana na kisiwa hicho, kisha Uingereza iliichukua mnamo 1810, na ukoloni wa kiingereza ndio mrefu zaidi katika historia ya kisiwa cha Mauritius.
Mnamo mwaka wa 1967 Mauritius iliunda uchaguzi mkuu, kisha ikaanzisha katiba mpya, na kutangaza uhuru wake kutoka kwa Ukoloni wa Uingereza mnamo Machi 12, 1968, na jamhuri likatangazwa baadaye mnamo Machi 12, 1992.
Mauritius inazingatiwa moja wapo ya nchi zinazoongoza barani Afrika, basi tangu uhuru wake, inaishi pamoja na maisha yenye utulivu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, kwa kuwa ina uchumi hodari wa ushindani, maisha ya demokrasia yenye mafanikio, pamoja na utamaduni tajiri na tofauti unaokuwepo ndani ya nchi.
Misri na Mauritius huunganishwa kwa mahusiano bora , ambapo kuna ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja tofauti na mabadilishano makubwa ya kibiashara, na misaada na kozi za mafunzo zimepangwa kutoka upande wa Misri katika nyanja nyingi kulingana na mahitaji ya upande wa Mauritius.