Wanaume Karibu ya Rais Abdel Nasser(4)... Balozi Mahmoud Riad, Mshauri wa Rais wa Masuala ya Kisiasa
Imetafsiriwa na/ Abdelmenem Khalefa
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed
Mahmoud Riad amezaliwa mnamo tarehe Januari 8, 1917, kwenye Mkoa wa Dakahlia, na baba yake alikuwa mhandisi. Alijiunga na Chuo cha Kijeshi nchini Misri mnamo mwaka 1934, akahitimu miaka miwili baadaye, akasoma huko, kisha akajiunga na Chuo cha Wafanyakazi na akapata cheti chake mnamo mwaka 1943, na akarudi kufundisha katika Chuo cha Kijeshi.
Riad aliacha kufundisha na aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Kijeshi huko Gaza mnamo tarehe Agosti 1948. Ingawa alihitimu kutoka Chuo cha Kijeshi, alijiunga na siasa mapema, kama alishiriki kama mjumbe wa ujumbe wa Misri katika mazungumzo ya Rhodes mnamo tarehe Februari 1949, na aliongoza ujumbe wa Misri katika Tume ya Pamoja ya Silaha kati ya Misri na Israeli kati ya (1949-1952), na baada ya mapinduzi ya Julai 23, 1952, akawa mkurugenzi wa Utawala wa Palestina na kuwajibika kwa masuala yote ya suala hilo katika Amri ya Jumla ya Majeshi.
Alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Kiarabu katika Wizara ya Mambo ya Nje mwaka 1954, na mwaka uliofuata aliteuliwa kuwa balozi wa Misri mjini Damascus, na kushiriki na ujumbe wa Misri katika kusaini umoja na Syria chini ya jina la "Jamhuri ya Kiarabu" mnamo mwaka 1958.
Nasser alimchagua Riad kuwa mshauri wa masuala ya kisiasa kati ya mwaka 1958 na 962, na kisha akahamia Marekani kama mwakilishi wa kudumu wa Misri katika Umoja wa Mataifa.
Alirudi Misri kuchukua nafasi ya mambo ya nje katika kipindi cha (1964-1972), kabla ya kuteuliwa tena kama mshauri wa masuala ya kisiasa, lakini wakati huu na Rais Anwar Sadat mnamo mwaka 1972. Mahmoud Riad alikuwa hatua muhimu katika historia ya Misri, alikuwa mmoja wa wanasiasa wenye uelewa mkubwa wa mgogoro wa Waarabu na Israeli, alikuwa kama mwamba uliowekwa na alibakia kujitolea kwa uelewa sahihi wa Azimio la 242, linalotaka kuondolewa kwa Israeli kutoka kwa maeneo yote yaliyochukua katika uchokozi wa 1967, kwa hivyo alikuwa mmiliki wa shule ya diplomasia, mawazo na utafiti wa kina.
Mnamo tarehe Juni 1972, Balozi Mahmoud Riad alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, akichukua nafasi ya Abdul Khaliq Hassouna, na alikuwa na kiapo hiki (naapa na Mwenyezi Mungu kuwa mwaminifu kwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na kufanya kazi yangu kwa uaminifu na heshima).
Wakati wa uongozi wake, mikutano ya sita, saba, nane na tisa ya kawaida ilifanyika, na wakati wa uongozi wake mkutano wa kilele wa vyama sita ulifanyika Riyadh katika kipindi cha kuanzia tarehe 16 hadi 18 Oktoba 1976, na alijiuzulu kabla ya mkutano wa kumi, hasa mnamo tarehe Machi 22, 1979, na barua yake ya kujiuzulu ilijumuisha kwamba hakuweza kuchukua majukumu yake baada ya hali ya Kiarabu kufikia kiwango ambacho hakiendani na malengo yake katika kufikia umoja wa hatua za Kiarabu, na hii ilitaka kustaafu kwake kutoka kwa kazi ya kisiasa.
Yeye ni mwandishi wa vitabu kadhaa, maarufu zaidi ambayo ni kitabu chake "Kumbukumbu za Mahmoud Riad" kilichochapishwa katika vitabu viwili, na "Utafutaji wa Amani na Migogoro katika Mashariki ya Kati", pamoja na makala nyingi na utafiti wa kisiasa uliochapishwa katika magazeti na majarida mengi.
Kazi hiyo ndefu ilimwezesha kuwa karibu na kushuhudia hatua muhimu na wakati, ambazo baadhi yake alizitaja katika kumbukumbu zake, zilizokuwa na kichwa cha habari "Utafutaji wa Amani na Migogoro katika Mashariki ya Kati", na kati ya matukio aliyoyataja, yalikuwa mvutano unaoendelea katika uhusiano kati ya Nasser na Marekani, haswa katika utawala wa Rais wa Marekani Lenden Johnson, aliyechukua uamuzi wa kukata misaada ya kiuchumi kwa Misri, Riad aliyochukulia "hatua ya Amerika iliyofungua njia ya Vita vya Juni."
Riad anasimulia ushuhuda wake, akisema: "Usiku ambao Gamal Abdel Nasser alijifunza kuhusu kukatwa huku, nilikuwa naye nyumbani kwake alipotoa maoni: 'Nani anayemuelewa Johnson, matatizo ya Amerika katika eneo hili sio kwa sababu ya mtu wa Gamal Abdel Nasser au nchi inayoitwa Misri, lakini matatizo ya Amerika ni kwa sababu ya sera ya Amerika mwenyewe, ni nzuri tu katika kushughulika na mawakala kama Camille Chamoun, ambaye aliondoa majeshi yao kwa sababu yake huko Lebanon mnamo 1958, na Shah wa Iran, ambaye alimfanya kuwa mshirika na Israeli dhidi yetu. Jamii ya Marekani ni imara na kubwa, lakini walituletea rais ambaye anashughulika na mantiki ya majambazi na watu wanaoishi katika karne ya ishirini."
Riad anaona kwamba mazungumzo binafsi ambayo aliyakusanya na Abdel Nasser, yalikuwa utangulizi wa moja ya hotuba zake kali, alizotoa huko Port Said mnamo tarehe Desemba 13, 1956, ambapo alisema maneno yake maarufu, "Wamarekani wanakunywa kutoka baharini, na ikiwa Bahari Nyeupe haitoshi kwao, wana Bahari ya Shamu."
Kuhusu msimamo wa Riad kuhusu hotuba hiyo na tathmini yake ya sauti ya Nasser, alisema: "Usemi kama huo bila shaka ulikuwa mkali katika kushughulika na nguvu kubwa kama vile Marekani, lakini Nasser ni mtu wa mapinduzi, na aliamini kwamba nguvu zake kuu haziko katika nafasi yake rasmi kama rais wa jamhuri, lakini kwa imani ya mtu huyo mitaani katika ulimwengu wa Kiarabu ndani yake, na katika uwezo wake wa kumchochea na kumhamasisha kwa kiwango maarufu; Hakulazimishwa kuwa mkweli kwake kuhusu ukweli wa hali hiyo bila kutumia diplomasia ya utulivu ndani ya ofisi zilizofungwa.
Wakati wa kazi yake, Balozi Mahmoud Riad alipokea mapambo mengi, alifariki dunia mnamo tarehe Januari 24, 1992.
Vyanzo
Kumbukumbu ya Mahmoud Riad
Tovuti ya Jumuiya ya Kiarabu
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy