Quett Masire... Mojawapo wa Marais Maarufu wa Jamhuri ya Botswana

Quett Masire... Mojawapo wa Marais Maarufu wa Jamhuri ya Botswana

Imetafsiriwa na/ Kamal Elshwadfy
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed

Quett Masire, Rais wa zamani wa Botswana, mojawapo wa wanasiasa maarufu, na mojawapo wa marais wake bora, amezaliwa Julai 23, 1925. Alihudumu kama Rais wa Jamhuri ya Botswana kama Rais wa pili wa nchi kuanzia tarehe Julai 13, 1980 hadi Machi 31, 1998.

Dkt. Masire alikuwa na jukumu muhimu katika uhuru wa Botswana, kupitia Chama cha Kidemokrasia cha Botswana, ambapo aliongoza ukuaji wa uchumi nchini Botswana wakati wa utawala wake, unaochukuliwa kuwa moja ya vipindi vya utawala wa uaminifu katika bara la Afrika, alilomaliza kwa kuacha urais kwa hiari mnamo mwaka 1998.

Baada ya kumalizika kwa utawala wake, alishiriki katika juhudi za maridhiano na ufuatiliaji wa uchaguzi katika nchi nyingine za Afrika. Mnamo mwaka 2007, alianzisha taasisi inayotaka kueneza maendeleo nchini Botswana na kanda hiyo, pamoja na kuchangia kutafuta suluhu ya amani ya changamoto zinazozikabili nchi kadhaa za Afrika kama vile Afrika Kusini, Msumbiji, Namibia, Zimbabwe, Angola, Ethiopia, Somalia, Lesotho na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Alifariki dunia mnamo tarehe Juni 23, 2017, katika hospitali moja huko Gaborone, kwenye mji mkuu wa Botswana, akiwa na umri wa miaka 92.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy