Sarah Sarahi Ngomo.. wa kwanza aliyeanzisha Chama cha Uuguzi katika Afrika Mashariki 

Sarah Sarahi Ngomo.. wa kwanza aliyeanzisha Chama cha Uuguzi katika Afrika Mashariki 

Na: Crepso Diallo

 Tangu Muda mrefu kabla ya "kubuniwa"  mashirika yasiyo ya serikali " NGao's" yanayohusika na usawa wa kijinsia na haki za wanawake na watoto, tayari walikuwa wamepata maendeleo makubwa katika hali halisi kuhusu masuala hayo mnamo siku za kabla ya uhuru. Sarah anazingatiwa kuwa miongoni mwa mamia ya wanaharakati wasio wa kawaida ambao wanajitenga na vile vya kawaida, vigezo, na mifano tayari ambayo hawajatendewa haki na historia. Alikuwa na jukumu kubwa katika kupambana na  ukoloni wa Waingereza na ubaguzi wa rangi nchini Kenya, na aliunga mkono haki ya elimu na upigaji kura wa uchaguzi kwa wanawake, licha ya  aliwahimiza Wakenya kujikomboa kutoka mila za kijadi zinazoathiri afya zao (tohara na ndoa za utotoni).

Sarah ni mwanamke wa kwanza Mwafrika aliyeruhusiwa kufanya kazi za uuguzi katika hospitali za tawala za kikoloni ambapo alianza shughuli zake kwa kuanzisha kampeni dhidi ya ukeketaji katika eneo la Kikuyuland, mwishoni mwa miaka ya thelathini na mwanzoni mwa arobaini, na alifanya kazi katika hospitali huko katika maeneo  ya mbali kwenye Afrika Mashariki "Kenya, Tanzania, Uganda" mnamo kipindi hiki  amepata mwaliko  ili kuhudhuria makongamano ya Pan Africanism kwa kuthamini juhudi zake za kuunganisha sekta ya matibabu katika Afrika Mashariki  kwa ajili ya kuanzisha hospitali za uwanja  ili kuunga mkono harakati za mapinduzi, na kupinga sera za tawala kali za kikoloni ambazo zilitenda dhidi ya wakazi wenyeji  kama ubaguzi unaohusiana na kupokea huduma za afya kutoka kwa madawa ،Hospitali na dozi za chanjo.

Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, alijiunga katika Baraza la Manispaa ya Nairobi, akaanzisha vituo vya utunzaji wa kijamii na kuanzisha programu za kutoa nasaha kuhusu wanawake na watoto katika maeneo ya makazi ya watu wenye kipato cha chini ikiwa mijini au vijijini.

Alifanya kazi katika Baraza la Ushauri la Afrika mjini Nairobi kuanzia mwaka 1949 hadi mwaka1951, mnamo kipindi hiki, alifaulu kunufaisha wanawake wakenya kama vile haki ya elimu,  kupiga kura katika mabaraza ya mitaa na kutoa mapumziko ya uzazi kwa wafanyakazi wa kike waafrika nchini kote, alitoa kauli ya kisheria  kwajili ya  haki za uzazi na utoto wa mapema. 

Katika upande wake wa kibinafsi, ana misimamo ya kishujaa pia alichochea kwa kutengeneza baiskeli ili kuepuka kupanda mabasi ya kibaguzi ambapo Wazungu walikuwa wameketi  juu ya viti vya fahari mbeleni wakati ambapo Waafrika wakiwa na viti vya mbao huko nyuma. vilevile,alitilia mkazo kuhusu kuwapa ruhusa ya kukaa mjini  kwa  familia ya Waafrika wanaotoka vijijini  ili kutumikia barazani ambapo imeshajengwa nyumba za watumishi wa halmashauri  katika sehemu  ambapo waafrika  hawaruhusiwi kuleta familia zao mjini.

Kwa sababu ya shughuli zake za kimapinduzi, ilifukuzwa kutoka Baraza la Ushauri la Afrika. akaunda Jumuiya ya Wanawake wa Afrika (AWL), ambayo ilifanikiwa kuwa mwamvuli uliojumuisha makada wa wanawake wa Kiafrika kadhaa katika mabaraza ya utawala ya kikoloni nchini Kenya, mpaka  chama hicho kikawa  kuitikia zaidi  mahitaji na maslahi ya Wakenya ili kuboresha hali ya maisha na nafasi za kazi kwa Waafrika na nguvu kubwa kwa ajili ya Kukomesha utawala wa kikoloni, kwa hivyo chama hiki kilikuwa  chama cha pili baada ya Mau Mau kilichotia wasiwasi  kwa utawala wa kikoloni nchini Kenya.

Mnamo Oktoba 20, 1952, ni siku ambayo chama cha Wanawake kilikuwa kimepanga maandamano mjini Nairobi, maafisa wa polisi wa Uingereza walivamia nyumba ya Sarah, wakamkuta akimnyonyesha mtoto wake, wakamtupa mtoto huyo chini na kumkamata, gerezani na licha  ya maumivu ya mateso alikataa kujiokoa kwa kutambulisha wenzake  au sehemu za kujificha za Mau Mau, hadi alikuwa  karibu afe kutokana  athari za mateso. vilevile , alinusurika kutoka kazi ngumu ambayo wafungwa walilazimishwa  kufanya, kama vile kuchimba mitaro ambamo mamia ya Wakenya waliuawa ikiwa walizikwa kwa siri msituni, wakati  ambapo"Sarah" akiwa gerezani, aliwafundisha wafungwa wenzake kusoma na kuandika, na kutibu walinzi kutoka kwa magonjwa ya zinaa.

Sarah, "aliachiwa " mnamo 1960, sio kwa  Nairobi alikokuwa akiishi kabla ya kukamatwa, lakini baada ya miezi 12 nyingine ya vikwazo katika kijiji chake "Kino ", ambapo alitakiwa kuja kwa kambi ya kiongozi  wa eneo hilo kila wiki. na baada ya kutekeleza  muda wa kukagua,  alijihusisha sana na shughuli za kisiasa na alichaguliwa kwenye  baraza la kusimamia sehemu ya  wanawake  kwa chama cha KANU mnamo Juni 1962.

Alimaliza Shahada ya Uzamivu kuhusu masuala ya usawa wa  kijamii na jinsia katika jamii za kiujamaa, ambapo alisafiri hadi Cuba, Umoja wa Kisovieti na Uchina.

Sarah alitengwa katika kipindi cha baada ya ukoloni  katika upande wa  ugawaji wa vyeo kwani inaonekana wazi  kwamba  sera za wahusika katika upendeleo zilionekana wazi kama jua, na kulikuwa na ushindani kwa  nafasi katika miundo ya uongozi inayotawaliwa zaidi na wanaume.

Sarah anachukuliwa kuwa mfano wa kimapinduzi aliyeenea kati ya maeneo ya mashambani na mijini, akiwa na upendo mkubwa sana kwa raia wake. Kiasi kwamba wakati wa safari za ndege kwa wanafunzi waliohamishwa miaka ya sitini , alipiga safari hadi Mashariki ya kati ili kusaidia wanafunzi wa Kenya waliokwama mjini Kairo.

Sarah Sarahi aliaga dunia mnamo Julai 14, 2003, akiwa na umri wa miaka 90, na hakuwa na chochote Duniani isipokuwa nyumba ndogo yenye sufuria tupu za kupikia.