Maadhimisho ya Miaka 81 tangu Kuanzishwa kwa Jeshi la Libya... Kwenye Nchi ya Misri Kulikuwa Kiini cha Msingi
Imetafsiriwa na/ Gerges Nagy
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed
Jeshi la Libya lilianzishwa kabla ya kuanzishwa kwa taifa la Libya lenyewe, yaani kabla ya ukombozi wa nchi kutoka kwa mkoloni wa Italia na kutangazwa kwa uhuru, yaani mnamo tarehe Agosti 9, 1940, baada ya Mfalme Idris Al-Senussi kukutana na viongozi arobaini wa Libya walioishi Misri kwa siku tatu nyumbani kwake Alexandria mnamo Oktoba 20, 1939, na mkutano huo ulichukua uamuzi wa kumuidhinisha Bw. Idris kujadiliana na serikali ya Kiingereza kuhusu kuundwa kwa jeshi ambalo kazi yake ni kushiriki katika ukombozi wa Libya kutoka kwa ukoloni wa Italia, na kwa kweli uamuzi ulitolewa kuunda jeshi la Libya, na kufunguliwa Ofisi ya kukubali kujitolea huko Kairo mnamo Agosti 12, 1940, inayojulikana wakati huo kama "Jeshi la Ukombozi au Jeshi la Senussi". Kambi ya kwanza ya mafunzo kwa jeshi la Senussi ilifanyika katika eneo la Abu Rawash huko Alexandria.
Jeshi la Libya lilishiriki katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia pamoja na vikosi vya muungano, na kupigana vita vyake vya kwanza katika eneo la Sidi al-Barrani la Alexandria mnamo Desemba 1940, na kuchukua bendera ya vita bila kujitegemea ya kuundwa kwa Jeshi la Uingereza la Nane, bendera nyeusi na nyota na crescent katikati, na vikosi vya Libya viliendelea kukimbilia baada ya mabaki ya Italia na Wajerumani waliorudi nyuma hadi walipoingia Cyrenaica na kisha Tripolitania, iliyokombolewa mnamo Januari 1943. Hadi mkoloni wa Italia alipofukuzwa kutoka Libya, Mfalme Idris Al-Senussi alitangaza kutoka kwenye veranda ya Ikulu ya Al-Manar huko Benghazi mnamo Desemba 24, 1951 uhuru na ukombozi wa nchi, na muda mfupi baada ya kutangazwa kwa uhuru, alisherehekea rasmi kuanzishwa kwa "Jeshi la Libya" mnamo Agosti 9, 1952, akitegemea kiini cha kwanza kilichoundwa Misri, mnamo Agosti 9, 1940.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy