Kufafua Bara Jeusi: Kutoka Kaskazini Hadi Kusini
Imeandikwa na: Alaa Yahia
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Tangu zamani, Misri imefuatilia sera thabiti na mwelekeo wazi katika mtazamo wake kuhusu bara la Afrika, ikijiona kama sehemu isiyotengwa ya bara hilo. Misri imejitahidi kujenga uhusiano imara na Afrika, ikichukua nafasi ya kuunga mkono bara hili dhidi ya ukoloni na kudai haki za watu waliokandamizwa na wakoloni. Kauli mbiu kama "Afrika yenye mapenzi ya uhuru na umoja" na "Afrika ni kwa Waafrika" zimekuwa msingi wa sera ya Misri kuelekea bara hilo.
Ni vyema kutajwa kuwa harakati za ukombozi barani Afrika na nafasi ya Misri, jina la hayati kiongozi, Gamal Abdel Nasser, haliwezi kupuuzwa. Alikuwa na jukumu muhimu katika kuhamasisha mapinduzi na harakati za ukombozi barani Afrika. Katika hotuba zake nyingi, Nasser alisisitiza kwamba Afrika na Misri ni vitu visivyotenganishwa, akisema: "Hatutaweza kujitenga na Afrika, na hata tukitaka, hatuwezi, kwa sababu sisi ni sehemu ya bara hili, na Mto Nile, ambao ni chanzo cha uhai wetu, unatoka moyoni mwa bara hili." Mapinduzi ya Julai 23, yaliyoanzishwa na Nasser, yalikuwa kama cheche zilizowasha mwenge wa ukombozi barani Afrika. Moja ya misingi ya mapinduzi hayo ilikuwa kuondoa mkoloni aliyekuwa akinyonya na kunyang'anya rasilimali za bara hilo.
Katika kipindi cha mapinduzi hayo, Misri ilichukua jukumu muhimu katika mafanikio ya bara la Afrika, hasa katika kipindi cha katikati ya miaka ya hamsini, ambapo wimbi la uhuru lilizinduliwa kutoka Kairo. Kabla ya mapinduzi hayo, nchi nne tu zilikuwa zimepata uhuru, lakini kufikia mwaka 1963, zaidi ya nchi thelathini zilikuwa zimepata uhuru wao. Mapinduzi ya Julai 23 yalichangia kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Afrika (OAU) lenye makao yake makuu Addis Ababa. Kwa mfano, nchi kadhaa zinaonyesha athari za mapinduzi haya kwenye uhuru wa Afrika:
Algeria:
Mapinduzi ya Julai yaliunga mkono wapigania uhuru wa Algeria, ambapo redio ya "Sauti ya Waarabu" ilikuwa msaada mkubwa katika kuhamasisha mapinduzi ya Algeria. Mnamo mwaka 1955, redio maalumu ilianzishwa kwa ajili ya kurusha matangazo kwa Algeria. Misri pia ilitoa msaada wa kijeshi, kifedha, na kisanaa kwa Algeria, na hata baada ya uhuru wa Algeria mnamo mwaka 1962, Misri iliendelea kuisaidia serikali mpya ya Algeria kurejesha utambulisho wake wa Kiarabu.
Sudan:
Mapinduzi ya Julai yalikuwa na jukumu muhimu katika kuhakikisha Sudan inapata uhuru wake baada ya mapinduzi ya Julai 1952. Misri ilihakikisha Sudan inapata haki ya kuamua hatima yake, na mnamo tarehe Januari 1956, Sudan ikawa nchi ya kwanza kutambuliwa na Misri.
Kenya:
Misri ilisaidia mapambano ya Kenya dhidi ya ukoloni wa Uingereza, ambapo harakati ya Mau Mau chini ya uongozi wa Jomo Kenyatta ilipata msaada mkubwa kutoka Misri. Misri ilianzisha redio ya "Sauti ya Afrika" iliyorusha matangazo kwa Kiswahili kwa ajili ya watu wa Kenya na wale wa Afrika Mashariki. Redio hii ilifichua ukatili wa Uingereza na mpango wake wa kuifanya Kenya kuwa nchi ya wazungu pekee. Misri ilihamasisha mapambano ya Kenya kwa njia mbalimbali, na viongozi wa harakati za kitaifa nchini Kenya walipata msaada mkubwa kutoka Misri.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo:
Historia inakumbuka jukumu la Misri linaloongozwa na kiongozi wake "Gamal Abdel Nasser" katika kuunga mkono uhuru wa Congo, na kusaidia watu wake mbele ya ukoloni wa Ubelgiji na washirika wake ndani ya nchi baada ya hapo; katika hatua zifuatazo, na Misri ilikuwa makini na utulivu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika msaada wa kudumu wa kisiasa, na hata msaada wa kijeshi, nchi zote mbili hunywa kutoka chanzo kimoja, ambacho ni Mto Nile, ambao vyanzo vyake vinaanzia eneo la Maziwa Makuu ambalo Congo iko, na kufikia Misri baada ya hapo kama chanzo cha uhai na maendeleo katika ardhi yake.
Afrika Kusini:
Misri ilichukua msimamo thabiti dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ilikemea sera ya ubaguzi wa rangi na kuondoa uwakilishi wake nchini Afrika Kusini. Nelson Mandela, rais wa kwanza wa Afrika Kusini baada ya kumalizika kwa sera ya ubaguzi wa rangi, alitambua mchango wa Misri katika harakati za ukombozi wa Afrika Kusini.
Mapinduzi ya Julai 23 yalikuwa kama mbegu ya kuanzisha Umoja wa Afrika, shirika lenye utulivu na uhuru wa kujitawala. Rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta, alisema: "Tutaendelea kumkumbuka Nasser kila wakati kwa sababu msaada wake kwa Afrika uliwakomboa watu wengi kutoka nchi zao."
Idumu Afrika... Idumu Misri