Taasisi ya Upangaji ya kitaifa

Taasisi ya Upangaji ya kitaifa ilianzishwa kutokana na Sheria Na. 231 ya 1960 kama taasisi ya umma yenye taswira muhimu ya binafsi ili kuboresha mbinu na mawazo ya mipango ya kisayansi nchini Misri kupitia shughuli za utafiti, mafunzo, za elimu, kukuza jukumu na kazi za Wizara ya Upangaji, kusambaza mawazo na kazi ya kupanga katika taasisi zote za kitaifa, na kueneza ufahamu wa kupanga katika jamii ya kimisri .
Na kama dalili ya jukumu la Taasisi katika kuunga mkono maendeleo ya kina nchini Misri tangu kuanzishwa kwake, basi Taasisi hiyo imeongezwa kwa uwezo unaohitajika wa kibinadamu na kimaumbile na imepeleka dhamini za masomo kadha kwa sehemu zote ulimwenguni ili kupata shahada za elimu katika nyanja mbalimbali. vilevile , tasisi ililetea wataalam wakuu ulimwenguni wenye utaalamu wa uwanja wa maendeleo na upangaji ili kuwasilisha uzoefu na maarifa kwa Taasisi, licha ya nyanja za ushirikiano na mashirika ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa ziliongezeka , pia taasisi kadha za kisayansi huko Ulaya, Afrika na Mashariki ya Kati. vilevile , Taasisi hiyo ilipewa uwezo wa kiteknolojia unaoendana na vigezo vya kisasa , ambapo taasisi hiyo ndiyo iliyokuwa na heshima na ilitangulia kumiliki kompyuta ya kwanza nchini Misri mwaka 1960.
na kupitia michango yake yote ya zaidi ya miongo mitano, Taasisi hiyo ilitoa nyongezo na michango muhimu katika nyanja za kazi yake na jukumu lake kuu . ambapo ilishirikiana na Wizara ya Upangaji katika kuandaa mipango na mikakati ya maendeleo mbalimbali , na katika kuainisha , kuchagua na kusoma miradi mikubwa, pamoja na kuunga mkono juhudi za mpangaji katika kushughulikiana na vipengele muhimu vya maendeleo kama: maendeleo ya kikanda, utafiti wa makazi duni, masuala ya mazingira na uendelevu , mipango ya jinsia , ushirikiano wa kibiashara na urambazaji kati ya nchi za Mto wa Nile, ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda na kimataifa, kuendeleza nafasi za kitaifa na mengineyo, vilevile , Taasisi inashirikiana na Wizara ya Upangaji katika kutekeleza miradi muhimu ya utafiti.
Katika uwanja wa Tafiti, machapisho ya utafiti ya Taasisi yalikuwa mengi na tofauti, ikiwa ni pamoja na mfululizo wa masuala ya mipango na maendeleo, maelezo ya nje, vipeperushi vya sera na hivi karibuni karatasi za sera.Machapisho hayo yalishughulikia masuala yote muhimu ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na maarifa wakati wa tangu zaidi ya miongo mitano, na Taasisi ilishirikiana na timu za utafiti zinazoshirikiana na wale waliofaidika kutoka shughuli za tafiti zake na wenye maslahi kutoka nchi ambapo wengi wao wanajulikana kwa ujuzi wa nyanja na mwelekeo wa kiutendaji.
Taasisi ilipata heshima na ilitangulia kuchapisha ripoti ya kwanza ya kitaifa kuhusu maendeleo ya binadamu katika ulimwengu wa Kiarabu mnamo mwaka 1993 na ripoti zifuatazo kila mwaka. Pia ilichapisha baadaye ripoti za kimaendeleo ya binadamu katika upande wa mikoa .Taasisi hiyo inazindua jarida maalumu la kisayansi nalo ni: Gazeti la Maendeleo na Upangaji la Misri.
Shughuli za machapisho ya utafiti na Gazeti la kisayansi zimeongezwa kwa harakati za kisayansi, kitafiti na kiutamaduni muhimu sawasawa kama : Semina ya Jumanne, Mkutano wa Wataalamu, Ufuatiliaji wa kitaaluma,Semina ya Watafiti Vijana,Semina za kisayansi, Mkutano wa mawazo wa kila mwaka, na nyinginezo zilizokutana pamoja ili kuwa na Sifa maalum za kitafiti kwa Taasisi kuu hiyo.
Katika uwanja wa mafunzo na ushauri, mafanikio ya Taasisi yasiyo na kifani , ambapo michango ya mafunzo ya Taasisi ilikuwa tofauti, na pande zake za kimkakati na zisizo za kijadi zilikuwa anuwai kwa lengo la kukuza maendeleo, vilevile, kujumuisha kategoria na sekta mbalimbali, kwa ushirikiano wa ndani , Kiarabu na wa kimataifa.
Miongoni mwa shughuli maarufu zaidi za Taasisi katika uwanja huo ni kutekeleza makumi ya programu za mafunzo mnamo kila mwaka katika mikoa ya Misri, Wizara na Taasisi za serikali, pamoja na mafunzo mbalimbali katika uwanja wa kompyuta. Diploma ya Taasisi pia ilichangia tangu miongo mingi katika kuunda uwezo wa maelfu ya vijana na viongozi wa Misri na nchi za Kiarabu na Afrika katika uwanja wa mipango na maendeleo. kuhusu upande wa masomo ya juu , tasisi ilishuhudia mabadiliko ya ubora hivi karibuni , kuanzia awamu ya Uzamili wa tasisi ya Upangaji na Maendeleo ambayo ikiidhinishwa na Baraza kuu la Vyuo Vikuu 2008 /2009, na kujiandaa ili kuanzisha utekelezaji wa programu ya Uzamili kwa ushirikiano na Taasisi ya Afrika ya Maendeleo ya Kiuchumi na Upangaji.
Tumegundua kuwa Taasisi tangu kipindi kizima cha kazi yake yenye shughuli nyingi, imekusanyika uzoefu na maarifa ambayo inaonesha faida za ushindani kwa muda wa kazi yake ndefu, kama vile: utaalamu wa utafiti wa utendaji, uundaji wa mfano, takwimu na akaunti za kitaifa, uzoefu wa kuunda data , taarifa na maarifa katika nyanja mbalimbali za upangaji na maendeleo, na uzoefu wa kuendeleza uwezo wa kusajili hati, akaunti ya kisayansi na maktaba za kina. Utandawazi , uwasiliano na ushirikiano wa tasisi pamoja na mashirika mengi muhimu ya ndani, kikanda na kimataifa ulichangia katika kuthibitisha uzoefu huo, na kuanzisha Taasisi ya Maendeleo ya Korea KDI, Taasisi ya Afrika ya Maendeleo ya Uchumi na Mipango IDEP, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Taasisi ya Kiarabu ya Upangaji , Taasisi ya Tunisia ya Mafunzo ya Ushindani na masomo ya Kiasi na nyinginezo, pamoja na mapokezi ya Taasisi hiyo kwa wataalam wengi wa kimataifa katika nyanja mbalimbali za maendeleo, na kuandaa makongamano mengi, semina, na majukwaa ya kisayansi na kifiria .
Kwa lengo la kuendeleza majukumu ya Taasisi, Sheria Na.31 , mwaka 2015 ilitolewa hivi karibuni kuhusu Taasisi ya Upangaji ya Kitaifa ili kuimarisha na kuthibitisha jukumu lake kama mamlaka ya umma yenye uhusika huru wa unaofanya shughuli ya kisayansi, na kama kituo kikuu cha kwa kufikiri juu ya masuala ya upangaji na maendeleo, na kuthibitisha jukumu lake katika kuendeleza tafiti na masomo yanayohusiana na uandaaji wa mipango ya maendeleo ya serikali na njia za kuitekeleza, na kusoma misingi ya na mbinu za kisayansi za kupanga na kuendeleza kwa lengo la ya kuwapatia wale wanaosimamia mchakato wa upangaji katika ngazi zote, watoa maamuzi na watunga sera kwa maoni na njia mbadala za kimkakati , na kueneza uelewano na ufahamu kwa masuala ya mipango na maendeleo ya kina na endelevu katika jamii. vilevile , sheria mpya ya Taasisi inakiri haki ya taasisi ama pekee yake au pamoja na wengine kwa kupatia shahada za kitaaluma: Diploma , Uzamili na Uzamivu katika nyanja za Upangaji na Maendeleo.