Hapa ni Afrika kutoka Kituo cha Utamaduni cha Afrika huko Aswan

Hapa ni Afrika kutoka Kituo cha Utamaduni cha Afrika huko Aswan

Imetafsiriwa na/ Mahmoud Ragab
Imehaririwa na kukaguliwa na/ Fatma Elsayed

Jengo la kistaarabu na  kitamaduni unaokupeleka kwenye ziara ya Kiafrika.  Unaweza kutembelea nchi za bara la Afrika; ili kufahamu mila na desturi za watu wake, kusafiri kwenye mito yake mingi, na kuangalia  misitu yake minene ya kitropiki na malisho ya Savanna yameenea kotekote.  Yote haya hayatakugharimu pesa nyingi, kuzuru makumi ya nchi za Kiafrika kama unavyofikiria ،lakini unahitaji tu gharama ya usafiri wako hadi kusini mwa Misri, ili Kutembelea Kituo cha Utamaduni cha Kiafrika ndani ya makumbusho ya Nile.

Mnara wa kitamaduni na kito cha usanifu  kiko upande wa mashariki wa Bwawa la Aswan kwenye eneo la mita za mraba 146,000, ikijumuisha mita za mraba 129,000 kwa maonyesho ya makumbusho. Inajumuisha majengo kadhaa, ambayo ni:
 Jengo kuu ambalo linajumuisha kumbi za maonyesho, ukumbi wa mikutano, maktaba, ukumbi wa watu muhimu zaidi , na ofisi za idara, pamoja na tovuti ya umma ambayo inajumuisha eneo la Maghreb Al-Oyoun, maeneo ya kijani, tamthilia  ya Kirumi wa wazi, uwanja wa pentagonal, jengo la shughuli za michezo, na maeneo mengine makubwa.  Jengo la makumbusho limepambwa kabla ya kuingia humo kwa kauli mbiu inayojumuisha nchi za Bonde la Nile zilizojumuisha Mto Nile, ikisisitiza ushirikiano kati ya nchi.Sehemu ya mwisho ya Mto Nile inawakilisha matawi ya Damietta na Rasheed, ikizungukwa na matone ya maji yanayowakilisha kila nchi  kutoka nchi ya bonde la Nile .

 Ua la makumbusho linapambwa kwa mitende ishara ya wema, ukuaji, uhifadhi wa maji, nguvu na ngumu, na 6 nakala za Mungu Hapi (mungu wa Nile kati ya Wamisri wa kale).
Chemchemi ya Bonde la Nile:
Hii ni kazi ya kisanii ambayo maji huanguka kutoka juu hadi chini kwa njia nzuri inaelezea mkondo wa mto wa Nile Kuanzia nchi za juu hadi nchi za chini ya mto, kazi hii inajumuisha ramani ya pande tatu za nchi za Bonde la mto wa Nile ambapo mto wa Nile huvuka kwake, na ramani hii inabebwa na Mungu Hapi.


 Kumbi za kituo

 Ukumbi wa Harusi wa Nile:

 Inajumuisha mwanamtindo wa Bibi-arusi wa Mto Nile; ishara ya utakatifu wa  Nile kwa Wamisri wa kale, na mifano miwili mikubwa ya Bwawa Kuu na Bwawa la Aswan, lililo na skrini zinazoonyesha hati zinazoelezea hatua za ujenzi wa kazi mbili, ili tuweze kuhisi kutoka kwao ukuu wa baba na babu zetu katika kujenga majengo mengi ya kuudhibiti Mto Nile; ili kutoa mahitaji ya maji ya nchi kwa nyanja zote.

 Ukumbi wa Bonde la Nile:

 Inajumuisha mwanamitindo wa  Waziri wa kwanza wa Umwagiliaji wa Misri " Ali Pasha Mubarak".Aliitwa Waziri wa Ujenzi.Alichukua wizara hiyo mnamo 1864 AD, Juu yake ni skrini inayoonyesha kazi ambazo zilianzishwa wakati wa utawala wake kwa kuongeza ofisi ambayo alitumia wakati huo.Pia inajumuisha maelezo kuhusu majengo mengi ya uhandisi kwenye Mto Nile, na ukumbi  unamalizika kwa maono ya siku za usoni ya nchi, mradi wa ekari milioni moja na nusu katika hatua zake tatu , na malengo ya mradi huu mkubwa.

 Msitu wa Afrika:

 Hii ni mfano mdogo kwa misitu ya Kiafrika, ikiwa ni pamoja na wanyama, ndege na mimea ambayo inawakilisha asili ya maisha inayopatikana katika misitu ya Afrika.

 Kituo hicho pia kina sekta tano zilizo kwenye ghorofa ya pili, ambazo zimegawanywa kulingana na mikoa ya kijiografia kwa bara la Afrika, ambayo ni: (Afrika Kaskazini, Afrika Magharibi, Afrika ya Kati, Afrika Kusini na Afrika Mashariki).

 Kanda ya Afrika Kaskazini:

 Inajumuisha nchi 6 katika ukanda wa Afrika Kaskazini: (Misri - Libya - Algeria - Tunisia - Morocco - Mauritania), na kinachofautisha eneo hili ni asili ya jangwa na hali ya hewa kavu.

  Kanda ya Afrika Mashariki:

 Inajumuisha nchi 14 katika ukanda wa Afrika Mashariki, ambazo ni: (Sudan - Sudan Kusini - Djibouti - Somalia - Ethiopia - Eritrea - Uganda - Rwanda - Seychelles - Comoro - Kenya - Tanzania - Madagascar - Mauritius).

 Eneo hili lina sifa ya asili yake ya kitropiki, kuenea kwa tambarare za Savanna na misitu minene, na ni makazi ya kundi kubwa zaidi la wanyama pori na wanyama wanaokula mimea kama vile: (Twiga, tembo, swala na pundamilia).

  Kanda ya Afrika ya Kati:

 Inapatikana katika eneo karibu na ua wa ndani, ikiwakilisha nchi 9 za ukanda wa Afrika ya Kati, na asili yake imetawaliwa na tambarare, Savanna, na misitu minene.Kanda hii inatazamwa na watafiti kuwa chimbuko la uwepo wa binadamu barani Afrika. Na ni maarufu kwa ueneaji wa misitu na maziwa.

  Kanda ya Afrika Kusini:

 Inajumuisha nchi za kanda ya Kusini mwa Afrika: (Angola - Botswana - Lesotho - Malawi - Msumbiji - Namibia - Afrika Kusini - Zambia - Zimbabwe - Swaziland), na sekta hiyo ni maarufu kwa wingi wa misitu, maziwa na visiwa.

  Kanda ya Afrika Magharibi:

 Inajumuisha nchi za Afrika Magharibi, ambazo ni: (Benin - Burkina Faso - Cape Verde - Côte d'Ivoire - Gambia - Ghana - Guinea - Bissau - Liberia - Mali - Niger - Nigeria - Senegal - Sierra Leone - Togo).

 Ni eneo lenye utajiri wa mabonde ya mito, kama vile mto wa Senegal na mto wa Niger, na lina sifa ya uwepo wa Savanna na wanyama wa porini.

  Mabonde ya mito ya Afrika:

 Ni sehemu ya mabonde ya mito ya Kiafrika, na inajumuisha paneli 6 kwenye mabonde makubwa ya mito ya Afrika.


  Ukumbi wa michezo wa nje:

 Inaweza kubeba watu 2,500,  sehemu ya nje ya Kituo cha Utamaduni cha Kiafrika, inaangalia Bwawa la Aswan katika panorama ya ajabu.

 Uangalifu  katika kuandaa Kituo cha Utamaduni cha Kiafrika huko Aswan na idadi ya skrini za kugusa katika kila ukumbi zinazotumia teknolojia ya mifumo ya habari.  Kupitia hiyo, wageni hutazama ramani inayoingiliana ya bara la Afrika, kutembea habari kuhusu nchi hizo, na pia kutazama filamu maandishi yaliyotafsiriwa katika lugha tatu (Kiarabu - Kifaransa - Kiingereza), karibu nchi 54 za Kiafrika, zinazotolewa na Wizara ya Umwagiliaji.

 Filamu za hali halisi zinaeleza eneo la kijiografia la kila nchi, mji mkuu, idadi ya watu, lugha rasmi, mila, desturi na dini, pamoja na jumla ya  pato la taifa, viwanda muhimu zaidi, maeneo ya watalii, na mabonde ya mito muhimu zaidi.

 Kuna skrini inayoonyesha filamu za katuni za wahusika Vero (kiboko) na Timo (mamba. Wanasimulia hadithi nyingi, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi mto wa Nile; kutokana na uchafuzi wa mazingira, harakati za maji ndani ya nchi za Bonde la Mto Nile, jinsi ya kuhifadhi maji, na uhusiano kati ya nchi za Bonde la Mto Nile).

 Ukumbi wa Maktaba ya kumbukumbu na Kituo cha Habari kilichoambatanishwa na kituo hicho kina vitabu vingi muhimu, hati  za kihistoria kuhusu nchi za bara la Afrika, na zimeunganishwa kielektroniki na maktaba kuu kwenye Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji huko Kairo.

 Kituo hiki pia kina kona ya makumbusho kwenye ghorofa ya chini, ambayo inajumuisha vitu vingi vya akiolojia, ambavyo vinarekodi safari ya mtiririko wa Mto Nile kutoka vyanzo vyake hadi mdomo wake katika Bahari ya Mediterania. Kona ya makumbusho ina pande mbili , (utawala - makumbusho. )

 Kituo hiki kinatofautishwa na ukweli kwamba kina vifaa vingi vya sauti vinavyosaidia watu wenye mahitaji maalum katika kushughulikia umiliki wa kituo hicho na kufasiri kwa Kiingereza.

Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy