Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kwenye Chuo cha Sayansi na Kilimo huko Tashkent, Uzbekistan mnamo mwaka 1958

Imetafsiriwa na/ Abdelmenem Khalefa
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed
Nakushukuru kwa mapokezi haya, yanayoonesha urafiki, na ninakushukuru kwa zawadi hii ya thamani, na kwamba Ibn Sina anajulikana katika ulimwengu wote wa Kiarabu, na vitabu vyake vyote vimeenea kwa Kiarabu, na kuna vitabu vya wanazuoni wengine wa kale huko Uzbekistan, na ninafurahi kuchukua vitabu vya wanazuoni wa Uzbekistan katika wakati huu wa kisasa.
Tunatarajia kufanya kazi ili kuimarisha ushirikiano na kubadilishana utamaduni kati ya Uzbekistan na Jamhuri ya Kiarabu. Waziri wa Elimu, Mheshimiwa Kamal al-Din Hussein, atafanya kazi ya kuimarisha mahusiano kati ya wanasayansi wa Umoja wa Kisovyeti na Jamhuri ya Kiarabu, na nadhani kwamba wanasayansi wa Kiarabu ambao wataongozana na Waziri watakuwa na maswali mengi.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy