Bibi Tahia Kazem, mke wa Rais wa marehemu Gamal Abd El Nasser, aliyebaki mbali na maisha ya kisiasa, na alikuwa mfano wa mwanamke wa kwanza na mama wa nyumba wakati huo huo, ambapo alimpa msaada na kuunga mkono kwa mumewe katika mielekeo yake ya kisiasa, na anapendelea kuzingatia maisha yake ya kibinafsi na ana kazi ya kuwalea na kuwatunza watoto wake, na hana chochote cha kufanya kazi kwa umma, ingawa hivyo, alipata kupendezwa na kushangaz kutoka wamisri.
Abd El Nasser alimjua kwenye jambo hilo huko Aleskandaria , ambapo kulikuwa na urafiki mkubwa kati yake na kaka wa Tahia, na Abd El Nasser alikuwa akielekea kuwatembelea nyumbani mwao pamoja na ami yake na mkewe, waliokuwa marafiki wa familia pia.Abd El Nasser alimpenda Tahia na aliomba kumposa , lakini kaka yake alikataa kwa mara ya kwanza kwa sababu ya kutoolewa dada yake mkubwa, na baada ya mwaka mmoja, Abd El Nasser aliomba tena ili kumposa Tahia baada ya ndoa ya dada yake, na kaka yake alikubali, posa ilitimiza , na miezi mitano baadaye harusi ilifanyika na ndoa ilitimizwa. Katika kumbukumbu zake, mwanamke huyo Bibi Tahia alisimulia yaliyosemwa na Abd El Nasser kuhusu ndoa yake akizungumza pamoja na watoto wake akicheka: "Mtu pekee ulimwenguni aliyeniamuru maneno na niliyakubali ni Abd El Hamid Kazem"."
Bibi Tahia aliandika kumbukumbu ambapo alizungumzia maelezo ya maisha yake na kumbukumbu zake pamoja na mumewe tangu walipojuana na alizungumzia juu yake kama mpenzi , mume na baba, na juu ya wakati wake naye kwa shughuli tofauti za kisiasa, na hivyo katika kitabu chake cha "Kumbukumbu na Yeye" kilichochapishwa na Dar Al-Shorouk mnamo 2011.
Tahia Kazim alizaliwa mnamo Machi 1, 1920 huko Misri, baba yake alikuwa mfanyabiashara wa mazulia , na aliishi na Rais Abd El Nasser hapo awali na baada ya kuchukua madaraka hadi kifo chake, akazaa na watoto wake watano nao ni : Mona, Hoda, Khaled, Abd El Hakim, na Abd El Majid. Alikufa mnamo Machi 25, 1992, na akazikwa karibu na mumewe kwa kutimiza matakwa yake wakati alisema siku ya kifo cha Abd El Nasser, "Nimeishi kwa miaka kumi na nane pamoja naye , sikujuali kwa Urais wa Jamhuri, wala mke wa Rais wa Jamhuri, nami sitaomba chochote baada ya hapo. Nataka kuniandalia mahali karibu na Rais, na ninalotarajia tu ni kuzikwa karibu naye".