Benki ya Maarifa ya Kimisri
Imetafsiriwa na/ Hasnaa Elsayed
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Kwa kuzingatia mpango wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri, ambao aliuzindua katika “Siku ya Sayansi mnamo 2014”, Kuelekea “jamii ya kimisri inayojifunza, inafikiri, na inavumbua”, na kama kuunga mkono juhudi za maendeleo ya jamii ya maarifa ya kimisri, ongezeko la hamu na shauku ya mmisri kwa sayansi, na kuunga mkono kwa elimu na utafiti wa kisayansi, Baraza Maalumu la Elimu na Utafiti wa Kisayansi lilianza kuchukua hatua ili kukamilisha mradi huu kupitia kufanya ziara za nje na za ndani, baada ya kujifunza mahitaji yote ya kijamii ya kimisri na soko la uchapishaji la kimataifa. Baada ya kutathmini aghalabu ya makampuni na mashirika yanayofanya kazi katika uwanja huo, mazungumzo yalifanyika ili kukamilisha mradi huu.
Benki ya Maarifa ya Kimisri ilianzishwa mnamo Januari 2016, kama mojawapo ya miradi ulio muhimu na kubwa zaidi ya maarifa ya kitaifa katika uwanja wa elimu na utafiti wa kisayansi katika historia ya kisasa ya Misri, pia Benki ya Maarifa ya Kimisri inatoa nafasi kwa wamisri wote wa kila kizazi, uwezo wa kufikia kiasi kikubwa zaidi cha maarifa na maudhuimada ya kitamaduni na ya kisayansi, yawe nisawa ya sayansi ya kimsingi, inayotumika, ya kiufundi, ya kibinadamu au ya kiutawala, pamojaidara, na vilevile vitabu vya jumla vya kitamaduni kwa ujumla, vikiwemo vitabu vinavyolenga watoto ili kuvitumika kupitia kompyuta zote, Pamoja na simu mahiri na kompyuta kibao nchini kote.
Benki ya Maarifa ya Misri inajumuisha milango mikuu miwili, kila mlango umegawanywa katika milango mingi.
Mlango mkuu wa kwanza :
Ni mlango wa upatikanaji wa habari, na mojawapo ya maktaba kubwa zaidi za kidijitali na kituo cha maarifa ya kielektroniki ulimwenguni kote, ambayo hutoa ufikiaji wa bure kwa machapisho ya kielimu na ya kisayansi katika matawi mengi ya maarifa kwa watu wote wa umma ndani ya Misri, kwa kujiandikisha kwa kutumia nambari ya kitaifa, barua pepe na data rahisi ya kibinafsi na ya kiutendaji, pia linatoa huduma zake kupitia milango minne ndogo kwa wasomaji, watafiti, wanafunzi, walimu na watoto.
Mlango mkuu wa pili :
Ni mlango wa uzalishaji na usambazaji wa taarifa za kitaaluma za kitaifa kwa vyuo vikuu, taasisi, vituo vya utafiti vya kimisri na taasisi yoyote ya kiutafiti au ya kitaaluma ndani ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kupitia mfumo wa uchapishaji wa kielektroniki wa kina, kwa mujibu wa viwango vya kimakisayan mlango huo unajumuisha mfumo jumuishi wa kuunga mkono uthibitishaji wa maudhui ya kiutambuzi, ya kisayansi na ya kiutafiti kwa vyuo vikuu vyote na vituo vya utafiti, ambayo inasaidia kumbukumbu ya kisayansi na kiutafiti ya Misri kupitia ifuatavyo :
- Mfumo wa usimamizi wa majarida ya kisayansi, kuyaorodhesha na kuyahifadhi kwa njia ya kielektroniki.
- Mfumo wa usimamizi wa mikutano, na unajumuisha uthibitishaji wa mashindano ya kisayansi, warsha za mikutano, usajili wa washiriki, usimamizi wa maonesho na usimamizi wa mfumo wa utiririshaji wa kazi wa uchapishaji.
- Mfumo wa kutathmini matokeo ya kisayansi ya ndani ya utafiti, kupitia mpango kamili wa kipekee ulioundwa kwa mashirika ya kisayansi kufuatilia na kutathmini majarida yao ya kisayansi ya ndani ya husika.
- Mfumo wa kuhifadhi na kujumuisha uzalishaji wa ndani kwa njia ya kitaifa kwa watafiti wote katika ngazi ya jamhuri.
- Kuhifadhi na kurejesha data zote kupitia mfumo mkuu pamoja na udhibiti mkali wa mfumo.
Benki ya Maarifa ya Kimisri pia inaendesha warsha nyingi maalumu na huduma za uchapishaji za kisayansi kwa ushirikiano na wataalamu wakuu na mashirika ya uchapishaji – na hivyo kwa mfano lakini sio tu – kwa taasisi, vyuo vikuu, wizara za nchi, pamoja na taasisi za majeshi ya kimisri.
Benki ya Maarifa ya Kimisri, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu na Elimu ya Ufundi, inatoa vyanzo mbalimbali vya Vyanzo vya habari vya kiutambuzi, vya kielimu na vya kiutafiti vilivyoandikwa kutoka kwa mashirika makubwa zaidi ya uchapishaji ulimwenguni, ambayo yanafaa kwa vikundi vyote vya umri, na vya kielimu kwa Kiarabu na Kiingereza, kuanzia hadithi za katuni na sauti za watoto, pamoja na duru za maarifa kwa sayansi mbalimbali na nyenzo nyingi za kielimu na vyanzo vya hati, na hata majarida ya kisayansi, vitabu maalumu, na utafiti wa chuo kikuu.
Kwa kuzingatia urekebishaji wa mfumo wa kielimu wa kisasa, Benki ya Maarifa ya Kimisri, inashirikiana na kampuni ya CDSM, kwa kuunga mkono mpango wa mabadiliko ya elimu ya kwenye kipindi cha awali cha chuo kikuu na kipindi cha chuo kikuu, unaolenga kuboresha matumizi ya kiteknolojia katika mchakato wa kielimu.
Na kama kuunga mkono mpango wa kiutafiti wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na uainishaji wa vyuo vikuu vya kimisri, Benki ya Maarifa ya Kimisri, imeshirikiana na Wizara ya Elimu ya Juu na Utafiti wa kisayansi na vyuo vikuu vya kimisri, imeunga mkono kuanza kwa kuzinduliwa mojawapo ya muhimu zaidi ya zana za kupima utendaji wa kiutafiti wa kitaaluma kupitia hifadhi data Scival, ambayo hutolewa na kampuni inayoongoza Elsevier kwa Wizara ya Elimu ya juu, utafiti wa kisayansi na vyuo vikuu vya kimisri.
Benki ya Maarifa ya kimisri hivi majuzi, kwa ushirikiano na kampuni ya Clarivate Analytics, na kampuni ya Dar Al Manzoumah, iliyoanzisha fahirisi ya kwanza ya nukuu za kimarejeleo kwa lugha ya Kiarabu “Arabic Citation Index”, ambayo ilizinduliwa mnamo mwaka 2021 kama sehemu muhimu ya ajenda ya Misri ya 2030 ya kubadilisha Misri kuwa “Uchumi unaotegemea maarifa”, na itakuwa ni taswira ya kwanza ya matokeo ya utafiti wa kisayansi kwa lugha ya Kiarabu kwenye faharasa ya kimarejeleo, ikiwa tu mradi uko tayari kutumia na kutafuta kwa Kiarabu na Kiingereza kwa ajili ya taasisi zote za kiutafiti na kitaaluma duniani kote kupitia Hifadhi data ya Mtandao wa Sayansi ( Web of Science), ambayo ni mojawapo ya wachapishaji wanaoaminika zaidi duniani na ndiyo pekee katika uwanja wa Kielezo cha manukuu ya marejeleo kisichotegemea upande wowote, na itasaidia kielezo cha manukuu ya marejeleo katika Kiarabu kwa ajili ya kutumiwa na watafiti nchini Misri na duniani kote.
________________________
Vyanzo:
Tovuti ya Benki ya Maarifa ya Misri
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy